Kwa nini serikali ianzishe miradi na kuishia njia, pengine kutumia muda mrefu kumalizika?

Ni jambo la kushangaza kwa serikali yetu sikivu pale utokeapo mradi kwa ajili ya wananchi, nachoweza kusema ni kuwa miradi yote inayoanzishwa na serikali yetu sikivu ya awamu ya Tano imekuwa ikiishia njiani pasipo kumalizika kwa muda ili wananchi wafaidike na huduma kupitia huo mradi,

Kipo choo hapo dar es salaam maeneo ya ilala (karume) mpaka leo kinajengwa na kusimama kwa muda wa kukaribia mwaka sasa.

Nauliza serikali inapoanzisha kitu huwa haina uhakika wa ni muda upi wa kumaliza hiyo kitu, au budget huwa inakataa na serikali yetu haipo makini?

Nawasilisha.

Sasa hicho ni choo tu je hayo mengine makubwa zaidi?

Trump alisema kweli tunamchukia bure tu

Mengne ndyo tusiombe kabisa, choo cha jiji kujengwa karibia mwaka ndgu kweli ni kisanga.

Alafu fatilia gharama za kiserikali ata kimradi cha laki sita lazima takwimu zao zitasoma b’s

Nimefuatilia ilo mbona halipingiki, halafu sasa hvi wamekuwa ni watu wa kukurupuka hatari, mimi nachoshangaa kitu kdgo kuchukua muda mrfu.

Serikali ya awamu ya 5 chini na huyu Daktati fake wa kemia ni dhaifu mno kuliko serikali zote zilizopita kuanzia ya mkoloni, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hivyo kutegemea mabadiliko chini ya huyu mshikaji ni sawa na kusubiri boat uwanja wa ndege

Tuvumilie tuu Mungu anatuona atatusaidia kwa hili… mbona nasikia sassa hivi anamepata kipyaaaa… kile kutoka kwa Ali Kiba kimetua mikononi mwake "DADA KASEMA’’

Unlock the codes plse.

Albadiri ndio inafanya kazi

Wanakwambia mambo mazuri yapo mbele kwa mbele.

Albadir watasema haifanyi kazi kwa kuwa haivuki boda.

Duuh.

Walaji na wezi ni wengi sana…

Mradi wa kawaida tuu kila mtendaji atautolea macho nae apate chochote…

Cc: @Mahondaw

Ha ha ha ha ina maana wewe bado hujapita kwa dada TAIFA? kule wazo kampata mdogo wake kutoka sehemu za Tandahimba Songea… Yule aliyepumzishwa kwenye advisory la Viaa Chukua Chako Murua

Ndoivo kila mfuatiliaji wa hiyo miradi kuanzia juu hadi chini anataka apatemo

Na ukitaka kujua angalia mradi wa magari ya BRT yako njiani kumalizikia… ama usubiri gari zaidi ya one hour ama ukute kituoni hamna tiket au laa basi msafiri bure… kwani aliyetuloga amefia bahari gani na alifungwa kwenye kiroba gani?

CHADEMA wana miaka 26 kwenye siasa za nchi hii hawana ofisi Katika jengo la kudumu na pia mwenyekiti ni Yule Yule mwaka wa 15 huu. Hayo ndio mafanikio tunayotaka.

CHADEMA imeingia je hapa mkuu wewe kweli una stroke na huenda inakula mshipa wa kufikiri… sogea huko