
Nimekuwa nikiwaona walinzi wa Papa wakiwa wamevalia mavazi ya aina yake, kuna wakati nikataka kujua huwa wanapatikanaje, ndipo nilipogundua kuwa ni lazima uwe na sifa fulani ili kuwa mlinzi wa Papa, katika sifa hizo, sina shaka kuhusu hizi sifa zingine kama: (1) Lazima uwe Mkatoliki; (2) Lazima uwe haujaoa; (3) Lazima uwe na umri wa kati ya miaka 19-30; na (4) Lazima uwe na urefu wa angalau sentimenta 175.
Lakini najiuliza kwanini ni lazima uwe raia wa Uswiss?...