Laana za mwanamke

Habari zenu!
Katika maisha ya kila siku ni kawaida kwetu sisi wanadamu kuwa na mahusiano na jinsia tofauti. Lakini pia katika mapenzi huwa malumbano ya hapa na pale hayakosekani. Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja.
Kuna rafiki angu alikuwa ni mkatili sana kwa wanawake, yani alikuwa n mtu laghai akishatumia anatemana naye tena kwa mabango ya kutosha. Lugha za kumuabisha Mwanamke kwake ilikuwa ni kawaida sana. Aliwafanyia hivyo wadada wengi sana na wengi wao alikuwa akiwaahidi kuwaoa kln waliishia kwenye majuto.
Aliendelea na tabia yake hiyo mpaka alipofikisha miaka 25. Katika umri huo alipata binti ambaye alikuwa anamjua Mungu. Binti alikuwa kaokoka. Kama kawaida ya jamaa alienda na sera zile zile za ndoa. Aisee binti wa watu kweli alitokea kumpenda yule jamaa. Wakaingia kwenye mahusiano, mambo yakawa mambo. Mpaka wakapeana tunda, jamaa hapo ndipo kichwa kilivimba sana. Ila sema kweli na jamaa alimpenda sana yule binti ambaye alikuwa mcha Mungu. Wakapanga kutambulisha kwa wazazi. Basi wakakubaliana kuwa siku ya Christmas kijana ataenda kwa wazizi yake na binti. Siku zikaenda ilikuwa mwezi wa 10 mara ikafika mwezi 12.
Nakumbuka ilikuwa tarehe za katikati ya mwezi wa 12 mwaka Jana binti akanipigia sim. Nilipokea kwa vile Mimi age imeenda sana nilisikia sauti ya huzuni sanaaa “shikamoo Shem” nikajibu marahaba wazima huko? Akijibu “wazima lakini huku mambo si mambo”! Duh! Tuliongea mengi sana na akaniambia kisanga kilichomkuta kweli nilipigwa na butwaa. Nikajiuliza mwanaume unapata wapi ujasili wa kumtukana mtoto wa kike matusi ya vile? Na kwa vile siku nilikuwa Sina bando la internet ilibidi nijiunge ili shem anirushie screenshots za sms zote za yale matusi ya jamaa.
Kweli ilikuwa ni aibu na fedheha yule binti dah! Kichwani nilijisemea Kama Mwanamke anakuudhi na kupelekea kumtukana namna hii acha niendelee kununua mijimama tu. Basi niliona zile screenshots zote duh! Zilikuwa ni maneno mazito kwa binti. Ila binti majibu yake yakuwa Kama ifuatavyo:
“Mungu anakuona”, “kumbe ndo tabia yako na ulikuwa unanidanganya”, “utanikumbuka tu” n.k sema kweli niliumia sana. Baada ya siku nilimwita yule Rafiki nikampa Counseling mpaka akamuomba yule mpenzi wake msamaha. Binti alikubali na maisha yanaendelea.
Ila mpaka leo jamaa kisaikolojia hayuko sawa kabisa huwa ananiambia kuwa akikumbuka mambo aliyomtendea yule binti anaumia sana. Wakati mwingine anatamani amwite mbele ya wazazi wake ili aombe msamaha before hajafa ila anaona aibu.
Karibuni kwa ushauri ili nimuokoe jamaa yangu.