Lengo la waasisi wa EAC linatimia..

Waanzilishi wa jumuia ya afrika mashariki walikua na lengo na tamanio kuona nchi za ukanda huu zikiwa moja kwa kila kitu.

Mafuriko ya watanzania kwenye blog hii ya Kenya ni kama ushahidi wa kutimia kwa tamanio la waasisi.

Wakati tukiendelea kuishi tamanio la waliotutangulia; tutumie nafasi hii kuonesha na kuukuza utamaduni wetu wa kitanzania.

Bado sana lile la kutawaliwa na madikteta wakirundi na kitutsi

Eac inazidi kuimarika; dhana ya “free movement” inaonekana hapa…

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

Kutimia lengo ni ngumi sana, labda tawala zibadilike zote mbili

Sioni ugumu wowote taratibu kama hivi tutakua Mahali pazuri tu

Kwanini mkuu??

Shida siyo sisi raia, bali ni jublee na ccm

Hatukuja Kenyatalk kwa bahati nzuri bali ni kwa bahati mbaya lakin tunashukur kuwa sehemu yetu ya kujihifadhi kwa muda.

Naona lengo linatimia

Jubilee imefanyaje mkuu Mimi huku mgeni.

Kabisa mkuu…

Malengo ya wstawaliwa yanatimia ila Malengo ya watawala mmh,mfano Kuna lile lenye rohombaya halioni hatari hata kuchoma vifaranga vya kuku vya majirani
Uhusiano huu linauchukia sana ila Ndo hamzidi Mungu.

Haaaa haaaa

Sioni uhusiano Kati ya hayo matamanio na kilichotokea Tanzania

Huo ni mtazamo wako mkuu unaruhusiwa kuwaza unavyoona sahihi.

Ukimbizi halikuwa lengo au tamanio la EAC. Kilichotokea huko TZ baada ya blog yao ya Jf kufungwa kwa sababu ya kukaidi kuisajili kwenye mamlaka ya nchi ili iwe inalipa kodi stahiki, baadhi ya wanachama wake wamehamia kwenye blog hii ya Kenya kama wakimbizi wa kidijitali. Wamepewa kijiji kama wakimbizi - they are e-immigrants sawa na wakimbizi wengine. Matatizo yao ya mtandao yakiisha watarejea kwao.

Ngogo kabla ya kuja ukimbizini si ulikuwa umekula ban kule nyumbani!?

Kumpiga chura teke ni kumwongezea kasi, tena wamefanya kosa kubwa maana kule home story ilikuwa inabalance maana kulikuwa na wafia chama, ila hapa ni mwendo wa kupewa makavu live tu

Hii sio free movement, labda kama hujui free movement. Huu upuuzi pia ndio umechangia hata wafanyabiashara kukimbiza mitaji yao nje ya nchi. Matokro yake makusanuo yameshuka imebaki kupika data , mikopo mingi inabidi kulipa mishahara. Huko ndio ziliko potelea 1.5t isiyo na maelezo. Nyie mliokuwa mnasifia sera mbovu na nyie mmejikuta huku uhamishoni na sisi wakosoaji. Anzisheni forum yenu ya kusifia maendeleo mnayohubiri tuje kuyaona.