Lipumba akili zake zarudi kwa muda

[SIZE=6][FONT=times new roman]LIPUMBA ASIKITISHWA UMASKINI KWA WANANCHI[/FONT][/SIZE]
[FONT=times new roman][SIZE=6]Na CLARA MATIMO, MWANZA[/SIZE][/FONT]
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2018/07/lipumba-300x230.jpg
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, ameishangaa serikali kwa kujinadi kwamba uchumi wa nchi unakuwa kwa asilimia 7.1 wakati wananchi wengi bado ni maskini.
Alikuwa akizungumza jijini hapa juzi katika kongamano la vijana wa chama hicho lililowahusisha vijana kutoka wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza.
Profesa Lipumba alisema serikali imeshindwa kukopa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania ili kuwakopesha wananchi waweze kupata mitaji ya kufanyia biashara.
Alisema kitendo cha serikali kuingiza katika bajeti baadhi ya miradi ambayo haikupitishwa na bunge kinayumbisha uchimu wa nchi.
“Hali hii inavuruga utaratibu mzima wa fedha za maendeleo ambazo hupitishwa na bunge kwa ajili ya shughuli mbalimbali ndiyo maana uchumi wa nchi unayumba.
“Huwezi kusema uchumi unakuwa wakati wananchi wako wengi wanamaisha duni na ni masikini,”alisema Lipumba.
Akizungumzia uchumi wa viwanda, Profesa Lipumba alisema ni sharti serikali iwezeshe wakulima kulima kilimo cha kutumia trekta badala ya jembe la mkono.
Alisema viwanda vinavyotakiwa kuanzishwa vitokane na mazao ya wakulima yakiwamo pamba, chai, kahawa na korosho.
Kuhusu demokrasia nchini, alisema kwa sasa nchi haiendeshwi kwa demokrasia bali inaendeshwa na kundi la watu au mtu mmoja mmoja ambaye hataki kukosolewa kwa malumbano ya hoja.
Alishauri ziundwe asasi ambazo zitasimamia utawala bora.
Akizungumzia ustawi wa jamii, alisema bado kina mama wajawazito hawapati lishe bora wakati wa ujauzito ndiyo sababu wengi wao wanajifungua watoto wanakufa na wengine wana utapiamlo.
Profesa Lipumba alisema CUF itamaliza tatizo hilo itakapoingia madarakani mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kushika dola.

Ipi?
Yake Au Ya Mtatiro?:smiley:

Ya Lipumba Mkuu

Mshenzi tuu yule.

Umaskini upi? Ameuona wapi? Mnona mambo yanaenda poa ?

Lipumba ni mchumia tumbo, hana jipya ktk fani Yake ya uchumi wala kwenye siasa. Lipumba ni “pepo” LA uhàribifu.

hv hawa wasomi kwanin wasijiajir watuoneshe mfano wa kuchukuo hiyo mikopo na kuanzisha hzo biashara dogodogo!

… mnafiki

Huyo mchumia tumbo,niliasha mpuuza kitamboo

Leo hii hata jiwe ukimtoa pale magogoni,ne ni shida tu nio maana yanakua majizitu.

Hawawezi kujiajiri,kazi kupiga porojoooo

Lipumba ni majanga.

duh kwel naanza kuamin wafanyabiashara wazur ni ambao hatujasoma

CUF ya Lipumba
CUF ya Magdalena

Hawezi kupona labda hajapewa dozi yake ya “fweza”

A failed professor