Lissu asimulia jinsi dereva wake alivyomfuata, anachofanya Ubelgiji

Saturday, September 8, 2018

[SIZE=7]Lissu asimulia jinsi dereva wake alivyomfuata, anachofanya Ubelgiji[/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4749534/highRes/2103363/-/maxw/600/-/ok2s83z/-/lissu+pic.jpg

[SIZE=5]Kwa ufupi[/SIZE]
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ameeleza jinsi alivyookolewa na dereva wake wakati akishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma, kubainisha kuwa dereva huyo kwa sasa yupo Ubelgiji na anasomeshwa na Serikali ya nchi hiyo
By Ibrahim Yamola, Mwananchi [email protected]
Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amemzungumzia dereva wake, Adam Bakari akisema aliondoka nchini kwa taratibu zote za kisheria na wala hakutoroka au kujificha.
Lissu alieleza hayo katika mahojiano aliyofanya na Mwananchi ikiwa ni mwaka mmoja tangu aliposhambuliwa kwa risasi, akisema dereva huyo hivi sasa anasomeshwa na Serikali ya Ubelgiji.
Mwanasiasa huyo alishambuliwa akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma, kabla hajashuka kwenye gari lililokuwa likiendeshwa na Bakari ambaye inaelezwa kuwa wakati risasi hizo zikimiminwa alihusika kumwokoa Lissu, kabla ya kutoka nje ya gari kujinusuru.
Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi, Lissu alisema, “Kuna wajinga wanaotumwa na watu wasiojulikana kueneza maneno ya kijinga kwamba dereva wangu anafahamu siri za kushambuliwa kwangu. Kwamba alitoroshwa na sasa amefichwa na Chadema na mwenyekiti (Freeman) Mbowe.”

Aliongeza, “Nimekuwa na dereva huyu tangu mwaka 2002 akiwa kijana wa miaka 19. Katika miaka yote hii amekuwa ni sehemu ya familia yetu. Ninamfahamu fika. Ninafahamu alivyo mwaminifu kwangu. Hawezi na asingeweza kufahamu njama za kuniua mimi halafu asiniambie.”
Alisema mara baada ya kushambuliwa na ‘watu wasiojulikana’ iliibuka minong’ono kuwa wakimpata dereva huyo wangekuwa wamemaliza maneno juu ya shambulio hilo.
“Watu wetu waligundua hatari kubwa aliyokuwamo dereva kutokana na minong’ono hiyo. Wakaamua kumtoa Tanzania na kumleta Nairobi nilikokuwa nimelazwa mimi,” alisema Lissu.
“Hakutoroshwa. Aliondoka na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na alipitia mpaka wa Namanga. Alipatiwa hati ya muda ya kusafiria na maofisa wa Uhamiaji Namanga. Wala hakufichwa Nairobi, alikaa na mimi Nairobi Hospital kwa miezi minne.”
Kwa mujibu wa Lissu, Jeshi la Polisi la Tanzania lilimjulisha kaka yake, Alute Mughway kuwa lingetuma wapelelezi kwenda Nairobi kuwahoji yeye (Lissu) na dereva wake. “Tuliwasubiri hawakuonekana mpaka wakati tunaondoka Kenya kuja Ubelgiji Januari 6,” alisema.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]“Dereva wangu hakutoroka Kenya kuja Ubelgiji. Ili aweze kusafiri kutoka Kenya alihitaji pasipoti ya Tanzania na viza ya Ubelgiji, hakuwa navyo. Hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ubelgiji ilimpatia hati maalumu ya kusafiria na kuingia Ubelgiji.”
Alisema, “Hapa Ubelgiji anaishi mji mmoja na mimi. Amekodishiwa nyumba na anaishi kwa gharama za Serikali ya Ubelgiji, si za Chadema wala za Mwenyekiti Mbowe. Anasomeshwa na Serikali ya Ubelgiji.”

Alisema bado dereva huyo anaweza kuhojiwa na wapelelezi kuhusiana na jaribio la mauaji dhidi yake akisisitiza kuwa utaratibu wa kufanya hivyo upo kisheria.
Mbali ya kuzungumzia suala la dereva wake, Lissu pia alitoa maoni yake kuhusu wimbi la wanasiasa hasa viongozi wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM akisema si jambo geni katika siasa za vyama vingi nchini au kwingineko duniani.
“(Lakini) sababu si ngumu sana kuifahamu, Watanzania wa sasa ni wapinzani kwenye mioyo yao. Wanataka haki. Hawataki kukandamizwa wala kuonewa wala kufanywa wajinga,” alisema.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Vilevile, Lissu alizungumzia ushiriki wa Mbowe katika matibabu yake kuanzia Dodoma hadi Nairobi akisema, “Msimamo wa Mwenyekiti Mbowe kwamba lazima nipelekwe Nairobi au Afrika Kusini, lakini si Muhimbili ndiyo uliookoa maisha yangu. Na siyo tu alihakikisha napelekwa Nairobi, yeye mwenyewe alilazimika kuacha shughuli za Bunge na za chama na kukaa nami Nairobi kwa zaidi ya miezi miwili kuniuguza.”
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Alisema Mbowe ndiye aliyeratibu michango na misaada ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani waliomchangia na kumwezesha kutibiwa hadi matibabu yalipofikia.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]“Mwenyekiti Mbowe ana nafasi kubwa, pengine kuliko mtu yeyote katika kuhakikisha niko hai hadi leo hii,” alisema Lissu.

[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Pia alizungumzia Serikali ya Kenya akisema ilitoa mchango mkubwa katika matibabu yake.
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]“Si tu nilipokewa Kenya kama mgonjwa, nilipewa heshima zote za (VIP) watu mashuhuri.”
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]“Nililazwa katika presidential suite (chumba chenye hadhi ya kirais) ya Nairobi Hospital kwa muda wote niliokuwa natibiwa hapo. Nilipewa ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi la Kenya kwa saa 24 kwa miezi yote minne ya matibabu yangu Nairobi Hospital,” alisema.

Kuhusu gharama ambazo ametumia kutibiwa mpaka sasa, Lissu alisema, “Hilo swali gumu kwangu. Gharama za Nairobi Hospital zipo Chadema. Za Ubelgiji sijazifanyia mahesabu lakini ni mamilioni mengi sana.”
[COLOR=rgb(226, 80, 65)]Mwananchi lilizungumza na mke wa Lissu, Alice kuhusu mwaka mmoja tangu kushambuliwa kwa mumewe na alisema, “Shukrani nyingi sana kwa upendo mkubwa ambao umemwezesha Tundu kupata matibabu anayostahili.”
Alice ambaye kitaaluma ni wakili alisema, “Japo ni miezi 12 sasa, nafarijika sana kuwa anaendelea kuimarika siku hadi siku.”

Safi sana…

Cc: @Mahondaw