Mabadiliko ya uongozi TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki)

Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, Rais wa Baraza ni Askofu Gervas Nyaisonga, Katibu wa baraza ni Padri Charles Kitima.

Kwani katiba yao inasemaje?

Okay…

Msingi wa hoja yako ni upi mkuu katika thread yako hii?

Mkuu nimeripoti kuwa TEC imefanya mbadiliko ya uongozi, ni kwa mujibu wa kanuni zao, uongozi hudumu kwa miaka mitatu. Kwa hiyo muda wa Rais aliyekuwepo Askofu Ngalelekmumtwa na Katibu wake Padri Sabaya umeisha.

Au ulitaka nisemeje boss?

Kitima huyu huyu?

Pamoja mkuu nimekupata, huyu Dr Rev Charles Kitima namkubali sana kwa misimamo yake isiyoyumba kwenye kutetea misingi ya haki, namkumbuka sana muda yuko St Augustine University Mwanza kama Makamu Mkuu wa Chuo

Naamini ni yule Dr Rev Charles Kitima alikuwaga St Augustine University Tanzania kama Makamu Mkuu wa Chuo, na kama ni yeye hakika Baraza limempata Katibu wake sahihi kabisa kwa nyakati hizi

Kitima ni jembe! Alipaswa kuwa hata Askofu.

Yes ndio yeye.

Tunashukuru kwa taarifa japo hatujui misimamo yao ni ipi …je wapo upande wa watawala ama wananchi.!

Dr Rev Charles Kitima anajulikana sana kwa misimamo yake inayoegemea kwa kundi kubwa la wanyonge

Kitima jembe,nyaisonga jembe TEC moto chini

Hivi Dr kitima bado ni padri tu. Warumi noma sana sio kama serikali ya Tz

Sina la kusema juu ya huyu Msomi, ni mtu anayejua nini anafanya.
Hapo TEC wamelamba dume.

Huyu Nyaisanga asije kuwaangusha wanambeya maana wanambeya kwa misimamo wanajulikana.

Team imetulia hakika Jiwe akae chonjo.

Muwe active kuripoti pia na kauli toka kwao ambazo hamtavutiwa nazo

kila mtu huandika anachokipenda!

[FONT=courier new]Hongera zake sana Mwalimu wangu na Former Vice Chancellor wangu SAUT Mwanza Fr. Dr. Charles Kitima. Nina imani kubwa sana nae na namwamini. Ndani ya ’ Ukatoliki ’ hakuna Watu wa ’ hovyo hovyo ’ bali kuna ’ Geniuses ’ watupu.

Proud to be a ’ Catholic '.[/FONT]

Mkuu samahani nisaidie. Askofu ni jukumu fulani au ni uwezo? Mfano ili ujue mantiki ya swali langu. Rais wa nchi ni cheo japo ni kiongozi wetu wote haimaanishi kuwa ndio mwenye akili au bora kuliko mawaziri au viongozi na wananchi wengine. Msingi wa hilo swali langu na mfano niliotoa ni kutokana na ww kusema angepaswa kuwa askofu n sio padre tu. Jitahidi usipotoshe na kama hujui kiri tu kwani tunahitaji kuelimika.

Kwasababu kumekuwa na upotoshaji au kujichanganya kati ya serekali na nafasi ya ukardinali. Kuna mtizamo serekali walikuwa wanadhani au kumchukulia Kardinali kama ndio mkuu wa kanisa katoliki hapa nchini, mpaka ulipokuja ufafanuzi kwamba kuna mkuu wa maaskofu hapa nchini na Kardinali ni muwakilishi wa papa ambaye ni askofu wa kawaida tu linapokuja utawala wa kimamlaka hapa nchini.

Don’t be naive pls. Hapa hatuko kubalance hadithi. Kila mtu anasema apendacho na kuchangia atakacho. Na hakuna anayekulazimisha ww kubalance unachopost hapa jukwaani. Nyie ndio wale wajinga mnaosema eti watu wanaikosoa tu serekali lakini mazuri hawasifii. Kama kuna mazuri changia upendavyo na wala sio kulazimisha hoja ziwe na + na -.