Magufuli asipomchukulia Makonda hatua jamii ifanyeje?

Ni Swali tu.
Tumepata ushauri wa kisheria kuwa Makonda katika sakata la makontena ametenda jinai mara nyingi
Ushauri wa kisheria toka kwa Tundu Lisu ni huu hapa
Moja, kama ni kweli kwamba makontena ya Makonda yana mizigo mingine (hapa imethibitishwa kuna masofa na hata tractor) ambayo hajaitangaza bandarini, basi Mkuu huyo wa Mkoa atakuwa ametenda kosa la jinai la kutoa taarifa ya uongo (false declaration) kwa mujibu wa Sheria mbali mbali za kodi za nchi yetu.

Hilo ni kosa la jinai pia kwa mujibu wa Sheria yetu kuu ya jinai, yaani Kanuni ya Adhabu, na kwa Sheria yetu ya TAKUKURU.

Pili, kama Mkuu wa Mkoa Makonda hajawataja hao marafiki au wafanya biashara(hili hajafanya) anaodai wamempa zawadi ya makontena hayo, hilo ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya TAKUKURU na Sheria ya Mapato ya Udhalimu (Proceeds of Crime Act).

Tatu, kama Mkuu wa Mkoa Makonda amepokea zawadi zinazodaiwa kuwa kwenye makontena kinyume na Sheria ya Misaada, Mikopo na Dhamana za Serikali uliyoitaja wewe mwenyewe, basi sio tu amekiuka masharti ya lazima ya Sheria hiyo. Atakuwa pia amekiuka masharti ya lazima ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhusu zawadi kwa viongozi wa umma.

Kwa makosa yote haya, haitoshelezi na haitatosheleza kwa Mkuu wa Mkoa Makonda kuambiwa alipe kodi anayodaiwa tu halafu yaishe.

Tujadiliane asipochukua hatua jamii ifanyeje???

Hawezi kumchukulia hatua Mkuu kwa kujua kwamba Bashite ndiye anayehakikisha amri za dikteta zitimizwe. Nani atekwe, ateswe na hata kuuawa. Hivyo dikteta hawezi kumuwajibisha Bashite zaidi ya kujibaraguza hadharani kwani anajua hatima ya Urais wake kwa sasa iko mikononi mwa Bashite na mbaya zaidi Watanzania hatuwezi kufanya lolote kwenye hili na Bunge uchwara nalo halikadhalika.

Kisamvu mororo kama kile atakipata wapi tena kama ataamua hivyo. Huyo ndo bimkubwa akifuatiwa na keti bila kumsahau angela huku mama jeska akisubiri kwa mbaaaali sana.

Keti? J…keti?

Hakuna linaloweza kufanyika, hata mje n uthibitisho wote…

Cc: @Mahondaw

Za asubuhi na za weekend to all family members.