MAMBO YA KUZINGATIA KIPINDI CHA UJAUZITO

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA MAMA KIPINDI CHOTE CHA UJAUZITO

Kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi yana tokea kwenye mwili wa mama na kufanya mabadiliko ya mwili Wake kwa kipindi cha miezi 9. Mara nyingi kuwa na hali tofauti kama kutapika, kichefuchefu na kujisikia mwili umechoka na uvimba miguu au uso n.k

Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa wakati wa ujauzito:

Kuudhuria klinik mapema

nivizuri mama akaanza kuudhuria klinik mapema ,pindi atambuapo anamimba sababu atafanyiwa kipimo vingi kwa kujua afya na maelezo ya kulea mimba yake. Na aendelee kuhudhuria mpaka pale atakapo jifungua

Lishe (vyakula muhimu wakati wa ujauzito)

mama hawezi kuzaa mtoto mwenye afya nzuri bila kula lishe bora , mama mjamzito lazima ale chakula chenye virutubisho mbalimbali vitakavyo mpa nguvu na afya kwake na mtoto.

Kula matunda ya kutosha, mbogamboga za kijani, mafuta na protein ipatikanayo kwa wanyama kama samaki,kuku na nyama ,kula vyakula jamii ya mbegu (maharagwe,njegere,Kunde,choroko,mbaazi n.k)

Mayai,maziwa,jibini(cheese),mtindi ,maboga,viazi,mihogo,magimbi,(ugali,wali na mkate) vyote hivyo unatakiwa ule kukuza mtoto na afya yako.

• Unywaji wa maji kwa wingi

mama mjamzito anatakiwa kunywa maji mengi wakati wa mimba humsaidia hutoa sumu mwilini na kutengeneza majimaji ya amniotic fluid kuwa ya kutosha ,yanayohitajika kwa ukuaji vizuri wa mtoto tumboni kwa mama.

kunywa maji humkinga mama mjamzito na magonjwa ya njia ya mkojo kwani mama mjamzito hupatwa na magonjwa ya njia ya mkojo kwa urahisi sana kipindi cha ujauzito. Hivyo maji kwa wingi huondoa hatari ya mama kupata UTI.

Maji hufanya ngozi yako iwe nyororo na kuvutia kunywa glasi 7 au 8 kwa siku na itakusaidia kuepuka kuapata stretch marks(michirizi)

• Tunza ngozi yako

Kutokana na mabadiliko ya mwili hormoni kuchangia mabadiliko ya ngozi ya mwanamke, kupata chunusiau mabaka meusi usoni au kifuani,nimuhimu kuzingatia usafi wa ngozi yako na kuifanya ionekane nadhifu kwa kutumia vitu asilia kama ,asali na ndimu ukichanganya ukapaka usoni mara 2 kwa siku,au utomvu wa alovera ikatokea mama anapata chunusi nyingi . Mama kupata michirizi (stretch marks) tumboni kipindi cha ujauzito kinachotakiwa paka mafuta mengi tumboni kama( cocoa butter,mafuta ya nazi au palmer oil) inasaidia sana kuepuka michirizi,usikune tumbo likiwasha,paka mafuta kwa wingi fanyia massage hapo utaepuka stretch marks.

• Fanya mazoezi
Ni muhimu kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ya aina mbalimbali ambayo ni mepesi na hayatokuwa na madhara kwa mtoto.

mazoezi kama ya Kutembea mwendo wa dakika 20-30 ufanye asubuhi na jioni ,

Mazoezi ya kunyoosha Mwili (stretching) au Yoga.

Mazoezi ya kuogelea

Ufanyaji mazoezi humsaidia mwili usichoke

Yanamsaidia mama kujakujifungua kwa urahisi.

Mzunguko wa damu unakuwa mzuri kwa mama.

Inamsaidia kupunguza uzito (unene)kwa urahisi,

Kuondoa uchovu wa mwili na kujisikia mwenye nguvu.

Utakapo ona dalili au mabadiliko yoyote usio yaelewa mwenye mwili wako wahi hospital.

Mama unaweza tokwa damu nyinyi,maumivu makali chini ya kitovu,pressure kupanda gafla,kupata homa kali,kuvimba miguu na mikono,kuzunguzungua , mtoto kutokucheza zaidi ya masaa 48 ,kutokwa maji mengi ukeni na dalili nyingenezo hatarishi wahi hospital.

• Mavazi

mama mjamzito anapaswa zingatia kuvaa mavazi mazuri yenye kusitiri mwili. uvaaji wa nguo za kubana sio mzuri utakuwa unafanya uchoke zaidi na kutokuwa comfort.Kwa wale wanaoishi nchi za baridi mnunue suruali zenye mipira tumboni special kwa mama mjamzito,hazibani unakuwa huru .

viatu virefu sio vizuri kwa mama mjamzito kwani huhatarisha maisha ya mama na mtoto. mama mjamzito anaweza kuanguka au kujikwaa ikakusabibishia kuanguka na kufikia tumbo na ukaharibu mimba (kusababisha kifo kwa mtoto tumboni) .

• uzito mkubwa(unene)

mama anatakiwa ahakiki uzito Wake kipindi cha ujauzito sababu uzito mkubwa ni hatari sana kwa mama na mtoto, hivyo mama zingatia kupima uzito wako mara kwa mara uendapo klinik iwapo utakuwa mkubwa utahitajika kuanza diet.

Epuka matumizi ya pombe na madawa ya kulevya(mihadharati)

unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya,au sigara ni hatari kwa mama na mtoto unaweza msababishia kifo,ulemavu,afya dhoofu,ukamzaa njiti, kuadhiri organs za mtoto n.k matatizo ni mengi sana ,mama jiepushe nayo.

Jipe mda wa kutosha wa kujipumzisha (kulala)

Urembo

swala la urembo nalo ni muhimu kuzingatia ili usiweze kupoteza urembo wako na usafi. Mimba inapendeza pale mama anapoonekana msafi na nadhifu,ukiwa kazini au upo nyumbani.Kwa wamama wa nyumbani baadhi wanajiachia sio vizuri haipendezi kutokujali mwili wako,kuna wengine hawataki kuoga wala kupiga mswaki hapo utampa wakati mgumu mzazi mwenzako,jitahidi kuwa msafi.

Sawa