masaibu ya hustler

so kuna time nilikosa job nikiwa msa na nilikua na rafiki flani mtaita anaitwa solomon tulimeet nikiwa kwa ile garage nilikua nafanya kazi,solo alikua boy flani mfupi,mtulivu shida yake alikua amemarry momo ingine size ya mamake.hii momo ilikua nyeusi kabisa halafu pia ni fupi,inakaa black rhino…according to SHILAWADU(Shirika La Wambea Duniani)huyu momo alikua poko ya pale club jamsa likoni na ilikua inaishi na beshte yake but day moja wakakosania client,momo ikafukuzwa,ilipofukuzwa ikaenda kwa solo kumuomba aspend night moja then kesho aende.IVYO NDIO SOLO ALIMARRY!
ALRIIGHT turudi kwa hekaya sasa mimi nikawa sina job nikashow solo anitaftie kibarua lakini akupata until idea ikatoka akanishow kuna place kunaitwa guranze au kasighau huko kuna madini niende nikachimbe kwa mgondi na akanihuk up na cuzo wake anaitwa peter. safari ikaanza kutoka Msa hadi samburu. .tukapanda matatu ingine kutoka samburu hadi vigurugani,hapo tukachukua nduthi hadi kilibasi,kufika kilibasi tukangoja zile lorry za makaa tukadandia hadi guranze.na tukalala hapo.kesho yake tukatembea kendu 25km hadi kacentre kanaitwa kwa Amina.hapo ndio migondi ilikua freestyle ukichimba mawe ni yako.(but siku iz kuna macartel) tukabuy unga na omena na tukaingia kwa mgondi mwenyewe anaitwa kauchimbe.life kwa migondi ni poa na ni mbaya… saa zingine unaeza chimba upate mawe mob ukue millionaire inna a day au uchimbe shimbo deep zaidi ya choo ukose kitu!..tukiwa huko kuoga ilikua sworn enemy…maji ilikua ya kupika na kukunywa,shida namba mbili ilikua wanyama especially ndovu,zinaharibu camps ama inakuanika juu ya miti.nakumbuka kuna jamaa tulikua camp moja msapere anaitwa mwangi aliumagwa na nyoka na ni usiku by the time tupate nduthi ya kumpeleka kasighau akadead.shida ingine ilikua watu walianza kukam na wife zao huko,juu hawawezi kamuana kwa camp wakaanza kuenda kukamuana kwa mashimo ya migondi na tustori twa chini chini zilikua madini hazipendani na tabia mbaya juu mahali kuna madini mostly uwa kuna mashetani.
Shida ingine ilikua kws,ulikua ukipatikana na nyama ya porini unachapwa kama mbwa koko ama place mnastay kupatikane mifupa mngechapwa hadi mseme ni nani aliua huyo mnyama.
huko porini still kuna wasomali wanalisha ngombe huko,nilijenga ubeshte na mmoja anaitwa abdi, msee alikua akinijenga maziwa ama saa wakichinja ngombe ananiita naenda kula nyama.he was my friend hadi siku moja alipatikana akichoma weed akatengwa na wenzake.akakam kwa camp yetu akajenga kanyumba hapo tukawa tunastay nae.hadi day moja wasee waliona gari ya mashifta ikikam wasee wote wakaingia porini,mimi nilikua nmedoz ilikua majioni,niliamshwa na mabrake,kuona ni mashifta nikitaka kukimbia abdi akaniita,nikasimama abdi akaingia nikidhani anatoka tuepe msee alitoka na rifle flani ya mbao na mtungi,akanishow nikihepa yeye ndie atanishoot! i didnt run, mashifta hawakutufanya kitu but walibeba maji na unga za wale wasee woote walihepa… acheni part 2 ikam badae

nice hekaya malizia

safi brathe

nilianza kukuheshimu na hekaya ya juzi kaka.umeyaona mengi

according to SHILAWADU(Shirika La Wambea Duniani)

according to SHILAWADU(Shirika La Wambea Duniani)
mimi bado sjaanza kuishi aki

Endelea

malizia hekaya buda

Enyewe umeona mengi wacha kuweka pause kwa hekaya

Black Rhino

hehehehehe…buda wewe umeona mengi kwa hii maisha

malisia kasee

Masaibu ya boi chaod

Nice hekaya.

Hekaya swaffi

waah si umeona mengi ya dunia hii

Kweli boy child upitia mengi…

Hekaya iko sasa kabisa. Ila tamatisha

Keep up bro. Nice hekaya wachananga na zile mzoga za kukopy paste.

Keep it coming man