Mashabiki wa Nchini Mexico waenda Russia na picha ya rafiki yao aliyekatazwa kwenda Russia na mke wake

[ATTACH=full]177153[/ATTACH][ATTACH=full]177154[/ATTACH][ATTACH=full]177155[/ATTACH][ATTACH=full]177156[/ATTACH]

Mashabiki hao waliamua kuchukua uamuzi wa kuchora picha ya rafiki yao ambaye wangeambatana naye kwenda Urusi kushuhudia Michuano ya kombe la Dunia ambapo timu yao ya Taifa ni miongoni mwa washirikii wa Kombe la Dunia.

Lakini rafiki yao hakuweza kwenda Urusi baada ya kukatazwa na mke wake na akaamua kutii amri.

Jana Mexico imecheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mabingwa watetezi Ujerumani ambapo Mexico iliibuka na ushindi wa bao 1 kwa nunge

Hahahahah watu wana vituko

Zile point tatu zao za jana hawawezi kujutia hivi vituko vyao

Jamaaa kashikwa mapembe. Ingekuwa bongo uyo mwanamke angeambulia kichapo na kurudi kwao

Kweli mkuu, halafu hawa rafiki zake wameonesha upendo wa hali ya juu sana hadi wakaamua wawe na picha kama kielelezo cha uwepo wa rafiki yao, Ona pale hadi wanaiweka picha kwenye kochi kama mtu kabisa

Wenzetu wakipendana ni upendo wa kweli sio kama wengine

Hao ndo marafiki wa kweli mkuu. Yaani uyo mke akiona hivyo nahisi atajisikia vibaya sana kwa uamuzi aliomfanyia mumewe.

Huku mtaani kwetu kuna jamaaa alimlamba mkewe vibao mpaka mkewe akataka kuondoka kisa tu alimzuia kwenda kuangalia mechi ya Juventus vs Real madrid

Wengi wetu hatuna subira na tunapenda kutosikia mawazo ya wanawake ambayo ukiongea naye vizuri mnaamua vizuri kwa pamoja.

Huyo wa kuzaba vibao sidhani kama alifanya vyema, angeondoka tu bila kumpiga mkewe ingekuwa bora zaidi maana hata kama wangekuja kununiana baadae jambo lingekuwa na kawaida tu

Wanaume siku zote tunajiona tupo sawa tu kimaamuzi

Angempa dozi Kali Kali mwezi mzima huyo wife na angemruhusu tu

Tunakosea sana, tulipoitwa sisi ni vichwa/viongozi wa familia sio kwamba maamuzi yote yawe ni sisi tu

hao jamaa nimewakubalii

atakuwa marioo

Kuna muda wanakera aisee, wao mara nyingi huwa wanawaza eti tukitoka mida ile tunaenda kupiga kazi za nje…

Cha ajabu ni pale unaweza kufunga DSTV, game za UEFA unaambiwa eti hawezi kulala peke yake wewe ukabaki sebuleni, nachekaga sana.

:p:p:p:p:p:p:p:p:p:p:p

Bonge la point umeongea mdogo wangu :p:p

Na hamtaki kushindwa…
Ila wanawake ni rahisi mno kuwaingia, tumia tu lugha ya kubembeleza mbona utaruhusiwa bila shida

Hahahahaaaaaa

Kwa mechi ya leo lazima kichimbike nikianza kuletewa hadithi za siwezi kulala peke yangu ukiondoka

Wanavyompenda rafiki yao naona wamemfunika na shuka la kimasai kabisa

Wanaume hawajawahi kuwa wanafiki kabisa. Natamani ningezaliwa mwanaume.

:D:D:D:D:D