Mashirika ya UMMA yanatishwa yatachangia hadi mitaji ili kumrithisha bwana mkubwa dictator kuwa ni gawio

Nimeiona hii huko JF wakajaribu kumshambulia ZZK. Rais ameonya kuwa yale mashirika ambayo hayatapeleka gawio(devidend) viongozi waachie ngazi. Matokeo yake hata yale dhoofu taabani wanajikongoja kupelela maduhuli wakiyaita gawio! jamani mashirika yatapona?
Na Zitto Kabwe
[ol]
[li]Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao[/li][li]ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.[/li][li]SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida.[/li][li]Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote.[/li][li]Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.[/li][li]Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi.[/li][li]Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio!.[/li][li]Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.[/li][/ol]
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.

Huyu jamaa mpuuzi sana

Yupi?

CHAMA CHA MAPINDUZI WAMETUFIKISHA MAHALI PABAYA…YANI WANAONGOZA NCHI UTAFIKIRI WANAONGOZA GENGE LA WAPIGA RAMLI

Mkuu, umeniwahi maana na mimi nilitaka kuuliza swali hilohilo…

Chungu kikuu kimekauka

Na tushaambiwa, hapendwi mtu hapa, inayopendwa pesa…

Cc: @Mahondaw

Magufool

Ni “Mega” mkuu, kutumia neno Magu unakuwa umemshushia hishima anayostahili!

mjifunze siku za usoni si kila aliyevaa kijani manapa kura zenu,haya oneni sasa

dah inasikitisga sana

Masahihisho Mkuu: Tujifunze siku za usoni tusikubali kutokuwa na tume huru ya uchaguzi.
Natubu kwa niaba ya judge Lubuva (kama Wakristo tunavyoaswa kufanya); maana hata yeye mwenyewe rohoni mwake anajua kuwa alichotangaza SICHO KILICHOKUWA