Mbowe: Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walipiga kura na kuzijaza kwenye maboksi. Hatutashiriki uchaguzi utakaoitishwa na NEC

Kutoka JF

https://www.jamiiforums.com/attachments/img_8576-png.870978/

HOTUBA YA MBOWE
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Majimbo ya Monduli na Ukonga, walishiriki kupiga kura na kuzijaza kwenye mabox kabla Mawakala wa Vyama vya Siasa hawajaruhusiwa kuingia ndani.

Kauli ya Rais kwa viongozi wake juu ya Uchaguzi imegeuka kuwa sheria kauli ambayo aliyoisema kuwa ampe Mkurugenzi Mshahara na gari halafu uje utangaze Upinzani umeshinda, tumeona madhara makubwa juu ya kauli hii.

Kwenye vituo cha kupigia kura makada ya Chama cha Mapinduzi wanakuwa ndio wasimamizi na ndio hao wanapika matokeo ya wapiga kura.

Katika Jimbo la Ukonga kulikuwa na vituo feki 16 vyenye wapiga kura 7,000 tumelalamika Tume lakini Tume imekuwa ikitupilia mbali malalamiko yetu.

Magari ya Serikali yamekuwa yakitolewa namba za usajili was Serikali na kuweka namba za usajili binafsi na kupewa wagombea wa CCM. Limefanyika hili Ukonga na Monduli.

Kamati Ndogo ya Kamati Kuu imefikia uamuzi wa kutoshiriki chaguzi zilizotangazwa na kwa sasa na badala yake tutapeleka nguvu kubwa kwenye oparesheni za kukijenga Chama kuliko kupoteza rasilimali nyingi.

Mbowe aliongelea juu ya kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwafanyia sherehe Polisi na kudai alistahili kuwa smegukuzwa kazi kwani wao ndio wanaochafua Majeshi yetu na kuleta mkanganyiko. Alisema kuwa, kosa hilo siyo la kukemewa tu kama alivyofanya Katibu Mwenezi, Humphrey Polepole.

Kwenye Vituo vya kupigia kura, Msimamizi wa Uchaguzi yuko kituoni na Makada wa CCM ili kuiba kura.
Ninafahamu kila anayerubuniwa kuunga mkono kusema kikwazo ni mimi Mwenyekiti na ningekuwa dhaifu CCM wangeshangilia sana lakini niwaambie sitopiga magoti kuwapa nafasi CCM kazi yao iwe rahisi.

Vyombo vya Habari vya Serikali vimekuwa vikitembea na Viongozi wa CCM na vimeacha kushughulika na matukio ya kijamii. Hata Bunge lililokatazwa kuonyeshwa mubashara kwa kisingizio cha kusema watu wafanye kazi lakini Rais anatembea na TBC watu wakiwa makazini pia.

Kelele za kuondoka kwa viongozi hakutatutoa kwenye reli. Kumbuka kila siku wanaingia wanachama wapya CHADEMA kwa maelfu, kama wanachama wa wa Chadema walionichagua wakitaka niondoke hata kesho nitaondoka, sio kwa kelele za CCM.


John Mrema

Tumaini Makene bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha kati tangu jana. Asubuhi hii Mawakili wamekwenda, Polisi wamesema bado wanaendelea kumshikilia wanachunguza kitu kinachoitwa Chademablog.com ambayo imesajiliwa na wanachama wetu wanaoishi Diaspora, wanataka Makene atoe hizo taarifa ambazo hana kwa sababu sio yeye aliyesajili.

Yaani hii ni hatari kuliko tunavyofikiria!

Hao NEC, tunawategemea Wasimamie kura kwa weledi, wao tena wanashirikiana na CCM kufanya huo uhuni??

Ni kweli kama alivyisema Mbowe, bila Tume huru hakuna uchaguzi Tanzania

Yaani full ujinga