Mdau, wadau, mshikadau.

#10
Neno mdau ninavyolielewa mimi na linavyotumiwa na wengi ni mtu mwenye maslahi na kiti fulani husika kinachozungumziwa, au ni mwanachama kindakindaki wa kitu fulani mfano mpira nakadhalika.
Alamsiki.
 
#11
@Meria Mata kila neno kishina chake huwa kina asili ya maisha ya kawaida ya binadamu. Kama unavoelewa Lugha uzaliwa kutokana na binadamu anavyopambana na mazingira yake ili aweze kuendesha maisha.

Mdau ama mshika dau kishina cha maneno hayo ni "Dau" Neno Dau ni neno lililokuwa linatumika kwenye tasnia ya uvuvi. Kwanza tuangalie dau hasa ni nini?

1529220408322.png
Hili ndilo Dau.

Dau lilitumika kusafirisha watu na mizigo na pia kufanyia kazi za uvuvi. Ili kujenga Dau ilihitajika wakati mwingine watu waungane ili kutengeneza ama mtu binafsi alikuwa anatengeneza na kumliki yeye mwenyewe.

Kwa ivo kulikuwa na wamiliki na waendeshaji wa Dau na wakati Dua likitoka safari ama kwenye kilindi cha bahari kuvua kulikuwa kuna kugawana mali iliyopatikana. Hapo ndipo neno Dau likaanza kutumika kumaanisha mali inayomilikiwa na mtu.

Ilikuwa ikisemwa "weka dau" au "toa dau" ilimaanisha mtu atoe kile alicho nacho na kukimiliki. Sasa baadae dau ikawa ni kielelezo cha mali anazomiliki mtu. Kwa ivo dau asili yake ni chombo hicho cha uvuvi na usafiri baharini.

Sasa mshika dau ni "stokeholder", mdau ni "Partner" na wadau ni wingi wa mdau! Kwa ivo mshika dau alikuwa ni mtu kwa mfano aliyetoa hela ama watu wa kuvua lakini yeye mwenyewe hamiliki Dau, na mdau ni yule alie kuwa kwa namna moja ama nyingine ni mshirika kwenye biashara ya uendeshaji wa Dau.
 
Last edited:

Top