Mdau, wadau, mshikadau.

Naomba nielezewe kaa mtoto mdogo wa miaka mitatu maana ya hizo majina.
Shukran

Mimi pia nimeingia darasa langu tu nikuskiza.

goja ni ite my new friend @joseverest aje atufundishe

Kuwa tayari na kamusi juu hata explanation ya maudhui hutaelewa hivi hivi.

Hii ni matusi bro au nini? looking for ways to use it

Hata mimi sijui maana yake niliskia mahali na sikuuliza nisionekane fala.

MSHIKADAU MIMI NIJUAVYO NI mtu mwenye hisa katika kampuni au shirika fulani.

MDAU NI mtu mwenye maslahi katika shughuli au kampuni fulani.

WADAU NI WINGI WA NENO MDAU

Dah! Hivi ni kumaanisha ndugu yetu uwesmeki ni mtu mwenye maslahi kwenye kampuni ya kwft? :smiley:

cc @Meria Mata

Mdau kwa kiingereza unaweza mwita shareholder au concerned part. wabongo tunaitana wadau. tukimaanisha wote tunahusika na nchi yetu. Sijui umeelewa mdau?

Neno mdau ninavyolielewa mimi na linavyotumiwa na wengi ni mtu mwenye maslahi na kiti fulani husika kinachozungumziwa, au ni mwanachama kindakindaki wa kitu fulani mfano mpira nakadhalika.
Alamsiki.

@Meria Mata kila neno kishina chake huwa kina asili ya maisha ya kawaida ya binadamu. Kama unavoelewa Lugha uzaliwa kutokana na binadamu anavyopambana na mazingira yake ili aweze kuendesha maisha.

Mdau ama mshika dau kishina cha maneno hayo ni “Dau” Neno Dau ni neno lililokuwa linatumika kwenye tasnia ya uvuvi. Kwanza tuangalie dau hasa ni nini?

[ATTACH=full]176734[/ATTACH]
Hili ndilo Dau.

Dau lilitumika kusafirisha watu na mizigo na pia kufanyia kazi za uvuvi. Ili kujenga Dau ilihitajika wakati mwingine watu waungane ili kutengeneza ama mtu binafsi alikuwa anatengeneza na kumliki yeye mwenyewe.

Kwa ivo kulikuwa na wamiliki na waendeshaji wa Dau na wakati Dua likitoka safari ama kwenye kilindi cha bahari kuvua kulikuwa kuna kugawana mali iliyopatikana. Hapo ndipo neno Dau likaanza kutumika kumaanisha mali inayomilikiwa na mtu.

Ilikuwa ikisemwa “weka dau” au “toa dau” ilimaanisha mtu atoe kile alicho nacho na kukimiliki. Sasa baadae dau ikawa ni kielelezo cha mali anazomiliki mtu. Kwa ivo dau asili yake ni chombo hicho cha uvuvi na usafiri baharini.

Sasa mshika dau ni “stokeholder”, mdau ni “Partner” na wadau ni wingi wa mdau! Kwa ivo mshika dau alikuwa ni mtu kwa mfano aliyetoa hela ama watu wa kuvua lakini yeye mwenyewe hamiliki Dau, na mdau ni yule alie kuwa kwa namna moja ama nyingine ni mshirika kwenye biashara ya uendeshaji wa Dau.

Aisee

Maudhui kwa kiingereza ni “content”

Thank you

Shukran Jazeera!

hio ni nini sasa
ile jazeera na jua ni Al jazeera news ya Qutar

Mdau naomba tukutane kwa uzi mwingine nafungua saa hii
nina maswali kadhaa

Hahaha Kiswahili kına kuwa

Kiswahili kifukuzwe