MOLA MREHEMU MAMA LUCY KIBAKI

Status
Not open for further replies.

Meria Mata

Village Chief
#1
Stolen.
A friend composed this in honour of Mama Lucy, thought I should share.

.
MOLA MREHEMU MAMA LUCY Kibaki.
.

Jamani yamenikaba, majonzi yanilemia,
Tanzia imetuzaba, tena Kenya tunalia,
Hii Leo dhoruba, mwendani metupungia,
Ya Rabi Mola Illahi, mrehemu Mama Lucy.
Ya Rabi Mola Illahi, mikono nimenyoosha,
Angaa nami niwahi, rambirambi kufikisha,
Ya Qudusi saa hii, maombi kufanikisha,
Ya Rabi Mola Wadudi, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi Mola wadudi, ni mazito lotukumba,
Sitofanya ukaidi, zaidi kwako twaomba,
Mpe mama afaidi, peponi apate nyumba,
Ya Rabi Mola Rahmani, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi ya Rahmani, poleni Wa Mukurwe-ni,
Mola awape imani, mutue nanyi nyoyoni,
Wakenya tumajonzini, yanamwelea manani,
Ya Rabi Mola Kudusi, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi Mola kudusi, wapoze wana Lucy,
Kagai siwe na wasi, Githinji nawe Judy,
Ziondoeni tetesi, sijakusahau Jimmy,
Ya Rabi Mola Latifu, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi Mola Latifu, mpe nguvu ba Kibaki,
Awe nao ukundufu, viondoke vyo visiki,
Mama likuwa turufu, alisimamia haki,
Ya Rabi Mola Karimu, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi Mola Karimu, meondoka muadhama,
Mefanya yalo muhimu, kusadia kina mama,
Wa ukimwi liudumu, kuwapa yaliyo mema,
Ya Rabi Mola Rahimu, mrehemu mama Lucy,
Ya Rabi Mola Rahimu, dua hii namwombea,
Mama Lucy mrehemu, huko nakoelekea,
Apate njema hatimu, Kenya kutuneemea,
Ya Rabi Mola Illahi, mrehemu mama Lucy,
R.Kizuka
 
#9
Why am I not feeling any sentiments whatsoever regarding thew dear departed? The first thing that came to mind on learning of her death was mbeca,govt money,my money...am I that insensitive? Iko chida
 
Status
Not open for further replies.