Msaada, mke wangu anateseka.

Kabla hajapata hili tatizo, hali yake ilikuwa nzuri kabisa.

Chanzo cha tatizo:
Alipata ajali ya baiskeli kwenye mteremko mkali wa mawe, alipakizana na mwanamke mwenzie kwenye hiyo baiskeli.

Tatizo linalomsumbua:
Akibeba kitu kizito kichwani anasumbuliwa na vitu vinne:
1: Maumivu ya kichwa,
2: Yatafuata maumivu ya shingo ya nyuma,
3: Halafu maumivu ya mgongo,
4: Halafu itafuata kubleed.

-Hii hali haiwezi kumletea matatizo ya kizazi?
-Hii hali inaitwaje kitaalam?
-Atumie dawa gani ili tatizo liondoke kabisa?

Ahsanteni.

Aende hospitali akafanyiwe vipimo na kupatiwa matibabu…

Haya matatizo ni makubwa mkuu. Aende hospital dokta akimchunguza atagundua tatizo zaidi kuliko huku tunasoma tatizo kwa maandishi.

Duh poleni

Ahsanteni kwa ushauri wakuu, nitampeleka hospitali.

Mpeleke hospitali…unaweza kukuta hilo la baiskeli sio lililosababisha tatizo

nenda jf og wapo doctors utapata msaada