Mtandao wa Kenyatalk kuwa tishio kwa utawala wa Magufuli

Serikali ya Tanzania chini ya utawala wa Magufuli imekuwa ikishtumiwa vikali na watu mbalimbali duniani kuwa imekuwa ikipambana kuua uhuru wa kujieleza na kutoa maoni kwa raia wake na vyombo vya habari vilivyopo nchini Tanzania.

Na mara kwa mara imekuwa ikivitisha na kuvifungia vyombo vyote vya habari vyenye mwelekeo wa kutoa habari za kukusoa utawala wa Magufuli.

Na tukio la karibuni kabisa ni kitendo cha mtandao wa kijamii wenye kuongoza kwa mijadala ya kisiasa na kijamii nchini Tanzania wa Jamiiforums kufungiwa ghafla.

Kwa sasa watanzania wengi werevu na makini hawaamini tena habari za kisiasa zinazotolewa na vyombo vya habari vilivyopo nchini Tanzania kwa sababu ya kulishwa habari za kutengenezwa na watawala ili kuwapamba.

Mwelekeo mpya ni kufuatilia habari kupitia mitandao ya kijamii, na kwa ghafla mtandao wa kijamii wa kenyatalk umegeuka kuwa kimbilio namba moja kwa watanzania waliokuwa wakifuatilia mijadala mbalimbali ya kisiasa na kijamii kupitia Jamiiforums.

Na taarifa za awali za ndani katika serikali ya Tanzania kuhusu hilo zimewashtua sana na kuhisi tayari watawala wa Tanzania wamepigwa chenga ya kimtandao na kasi ya kukosolewa iko pale pale.

Mikakati mizito huenda ikapangwa na watawala wa kitanzania katika kukabiliana na kenyatalk ili kufifisha uhuru wa kujieleza. Sijui wataanzia wapi na kupitia wapi, lakini ni lazima watajaribu tu.

Wait&Watch.

Malaika watakuja tu

Kiswahili kigumu kweli

Why don’t you TZ people use VPN to open new blogs and forums ?

Translate. Hiyo imewapita

Hii hapa itabidi umewasilisha ombi lako kwa kutumia Kiswahili

Watumie Google translator

Admean asipeleke makende TZ kusafisha macho na Baikoko. Hizo clawmatsu zitawekwa pingu

Huyo mmiliki wa JamiiForums hajui Bitcoin, Tor na VPN? Aglalikua kashaanzisha forum mpya untracable kwake by last week na kuhamisha kilakitu na kilamtu humo. Maxence Melo umeangusha watu wako mdau. Fanya hima

kiswahili kifukuzwe…aisee

does the law affect users? I mean if he launches a different forum, are the users also classified as “bloggers” meaning they need to pay that exorbitant amount to post?

hawa watanzania wanafanya nianze kukumbuka vile nilipafa D kiswahili KCSE

Admini Wa jamii forum yeye ni zuzu kwani hajui kuna brosa ya kitunguu ama mtandao mweusi

Hahahahaha. Mbona kiswahili kilichotumika hapo kuwasilisha mada ni cha kawaida sana na ni kirahisi!?
Ila tulikuwa na wakenya wengi kule jf tukijadiliana na kutanabashiana habari mbalimbali za ulimwengu, mwanzoni walikuwa wanapata shida sana katika upande wa sarufi, ila kwa sasa wengi wamekili kuwa jf imewafanya wawe watumiaji/wazungumzaji wazuri wa kiswahili.

He could launch a different forum, port all JF content n users there, while making sure the new one is not connected to him in any way. This is where Bitcoin, tor and VPN will be useful.

To circumvent the new TCRA rules, Tz users can use VPN, while international users can access it normally.

Itabidi tuwa tichi kiswahili

Acha ufala

Punguza ushamba ndugu yangu.
Hizo ni swaga za kizamani sana. Eti unataka kujionyesha unajua kiingereza kwa kujifanya hujui kiswahili!!!

Yaani mtu umezaliwa Kenya, tena kijijini kule ambapo wazazi wanajua kuongea kijaluo, kikikuyu, kiluo au kikamba tu, halafu wakaona na wewe upate Elimu darasani, ghafla unajifanya ulizaliwa uingereza, kisa umemudu kuandika na kusoma sentensi kadhaa za Kiingereza.

Kiswahili kinaweza kuwa lugha ngumu kwa mzungu, mchina au mhindi lakini kamwe kiswahili hakiwezi kuwa lugha ngumu kwa mbantu aliyezaliwa au kuishi kenya.

Kiswahili kifukuzwe ili tulete kikamba, kikikuyu au kijaluo?

Ukiondoa kiswahili kwa wakenya kitachobakia ni kikabila tu kwao. Kiingereza sio chao. Kiingereza ni lugha ya kuiga, kujipendekeza na kufichia ujinga tu.

Pale mjaluo anapojaribu kuwa fundi wa kiswahili kama mzaramu:D:D:D:D:D