Mtori wa ndizi

[SIZE=5]Mahitaji[/SIZE]
[ul]
[li]Ndizi bukoba 2 kubwa zilizokomaa vizuri[/li][li]Karoti 4[/li][li]Butter vijiko 2[/li][li]Kitunguu maji 1[/li][li]Nyama robo[/li][li]Supu ya nyama[/li][li]Maziwa robo lita[/li][li]Cream ya maziwa[/li][li]Mdalasini robo kijiko cha chai[/li][li]Nutmeg robo kijiko cha chai[/li][li]Nyanya 1[/li][/ul]

[SIZE=5]Maelekezo[/SIZE]
[ul]
[li]Bandika nyama jikoni, iive iwe laini na ibaki na supu.[/li][li]Menya ndizi, nyanya, kitunguu na karoti.[/li][li]Chukua sufuria, kata nyanya, ndizi, karoti na kitunguu. Weka vyote kwenye sufuria moja.[/li][li]Weka mdalasini, chumvi, butter na nutmeg kisha weka supu na nyama. Bandika jikoni.[/li][li]Supu ikikaribia kuisha, weka cream, punguza moto acha ichemke kama dakika 5 kisha weka maziwa.[/li][li]Epua, acha ipoe kisa saga. Ipashe kidogo mpe mtoto ale itakayobaki iweke kwenye jokofu.[/li][/ul]

Ndio maana @Babu Asprin hazeeki mapema kwa haya mahanjumati mujaarabu unayomuandalia

Ahsante sana bibi kwa somo la jikoni

Au hii ni ya watoto tu?

Hii ni menu ya babu baada ya usiku wa viti virefu

:p:p:p:p:p:p:p:p:p