MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Leo ni siku nyingine Bwana ametupa neema mimi na wewe kuiona, hivyo ni wajibu wetu kiutimia vizuri siku yetu kwa kujifunza maneno yake ambayo ndio nuru yetu na uzima wetu hapa duniani kila siku.

Leo kwa neema za Bwana tutajifunza juu ya huu mwaka wa Bwana uliokubaliwa ni upi ambao Bwana Yesu aliuzungumzia katika…

[INDENT]Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”.
[/INDENT]
https://wingulamashahidi.org/wp-content/uploads/2019/10/BreakChain_lg.250w.tn_.jpg

Sasa ni vizuri kufahamu kuwa biblia inaposema mwaka sio kila mahali inamaanisha kuwa ni mwaka Fulani mahususi labda 2018 au 2019 hapana, bali inamaanisha kipindi Fulani cha wakati kilichotengwa mahususi kukamilisha lengo Fulani chenye mwanzo wake na mwisho wake ambacho kimefananishwa na mwaka…

Hivyo hapo ni sawa na kusema “kuutangaza wakati wa Bwana uliokubaliwa”…Ikiwa na maana kuwa kama huo ndio wakati uliokubaliwa, basi pia zilikuwepo nyakati nyingine ambazo hazikukubaliwa…. Na pia tunapaswa kufahamu ulikubaliwa kwa kusudi lipi?

Katika agano la kale kila mwaka wa 50 uliitwa Yubilee, mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa maachilio, haikuruhusiwi kulima wala kupanda, ardhi ilikuwa inastarehe, ni mwaka ulioitwa mwaka wa maachilio ya watumwa, na kusamehe watu madeni yao (Walawi 25:11),

Na ndicho Bwana Yesu alichokuja kukifanya katika agano jipya, kuleta maachilio ya vifungo vyote, vya rohoni na mwilini, vile vile alikuja kuutangaza huo mwaka Bwana uliokubalika, yaani wakati wa Mungu kumkubali mwanadamu, kumwokoa na kumfunulia uso wake na mapenzi yake amjue yeye…Hiyo ililetwa na Bwana YESU tu peke yake, kumbuka hapo kabla Mungu alikuwa hampokei Mwanadamu yeyote haijalishi ni kuhani au nabii au rabi kiasi gani, hakukuwa na mwanadamu yeyote ambaye aliwahi kumkaribia Mungu na kutoa hoja zake pasipo kuwa na deni la dhambi ndani yake, na ndio maana ilimpasa kuhani mkuu peke yake aingie patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa mwaka afanye upatanisho wa dhambi za watu, pamoja na dhambi zake mwenyewe ambazo kimsingi zilikuwa haziondolewa bali zinafunikwa, baada ya hapo shughuli imeishia hakuna mashauri wala mahojiano, unaondoka mbele ya madhabahu ya Mungu ambayo ilikuwa duniani na wala sio mbinguni…

Lakini Bwana Yesu alipokuja yeye alisimama kama kuhani mkuu, na hivyo sasahivi sio tu tumepata ondoleo la dhambi na maombi yetu kusikiwa bali pia tunaketi na kula na kunywa na Mungu katika ulimwengu wa Roho kama vile Baba na mtoto wake wa pekee ampendaye… Haleluya!.

Kwahiyo tunaishi bado katika kipindi cha Mwaka wa Bwana uliokubalika…Lakini huu wakati hautadumu milele, mwaka Bwana uliokubalika hautadumu milele, kuna wakati Bwana Yesu kama kuhani mkuu atasimama kutoka katika kiti chake cha ukuhani, na kuanzia huo wakati na kuendelea hakutakuwa na rehema tena, na wala Mungu hatakuwa na nafasi ya kuwatazama waasi, kinachobakia tu ni ghadhabu ya Mungu kumiminwa juu ya waovu wote…Na huo wakati upo karibu sana ndugu, Unyakuo ukishapita tu basi fahamu kuwa kiti cha rehema kilishaondolewa…

[INDENT]Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba ATAKAPOSIMAMA na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
[/INDENT]
Na ndio maana biblia inasema wakati uliokubalika ndio sasa, ndio huu tulionao mimi na wewe, yaani leo kwasababu kesho hatujui itakuwaje….

[INDENT]2 Wakorintho 6:2 “(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”…[/INDENT]
Usisubirie wakati ambao haukubaliki ndio umkumbuke Mungu, utakuwa umeshachelewa ndugu. Ikiwa bado upo mbali na Kristo wakati ndio huu wa sasa tubu dhambi zako, jitwike msalaba wako umfuate YESU, atakusamehe dhambi zako, kisha hakikisha baada ya kutubu kwako unabatizwa kisha yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu bure kama alivyoahidi katika (Matendo 2:38)…

Bwana akubariki sana.

Whatsapp: +255693036618