Mwalimu Meru auawa na mpenziwe wa miaka miwili

INSERTER

Village Elder
#1
Polisi Meru wamemzuilia mwanamke wa miaka 28 kwa kumuua mpenziwe.

Marehemu alikuwa mwalimu wa Shule ya Upili Meru na familia yake haijafahamishwa.

Wawili hao wamekuwa wapenzi kwa miaka miwili Mwanamume wa miaka 29 aliyekuwa mwalimu Meru Jumamosi Septemba 30 aliuawa na mpenziwe wa miaka miwili baada ya kuhitilafiana.

Sababu ya mauaji hayo haijabainika lakini polisi walimkamata binti huyo, Faith Kanario kumhoji. Marehemu alikuwa mwalimu katika Shule ya Upili ya Meru Muslim Day. Alidungwa kisu shingoni, tumboni na kifuani na mwanamke huyo wa miaka 28 katika hoteli moja mjini humo.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho na walioongea na Kenya News Agency (KNA), wawili hao walikuwa wamekesha kubugia pombe kabla ya kwenda katika Hoteli ya Castella kupumzika. Mwili wa mwalimu huyo ulipelekwa katika mochari ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Meru huku polisi wakichukua hatua ya kuifahamisha familia.
 
Top