Mwanadiaspora uchwara na sifa uchwara kwa dikteta

[SIZE=5][FONT=times new roman]https://tsnapps.go.tz/public/uploads/73c086e71f79de5a8739ef1dfe3ba52b.jpg [/FONT][/SIZE]

[FONT=times new roman][SIZE=5][U]Utendaji wa serikali ya JPM unavyogusa zaidi Wanadiaspora[/U]
[U]Mwandishi Wetu[/U]

19/06/2018

JITIHADA za dhati za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais mchapakazi, Dk John Magufuli kuonesha kwa vitendo utekelezaji wa mipango ya kuwasaidia Watanzania kuinuka kiuchumi zinazidi kuungwa mkono na wananchi.
Nikiwa mmoja wa Wanadiaspora niliyeshiriki huko nyuma kuratibu makongamano ya wanadiaspora, safari hii nimepata mirejesho ya Wanadiaspora wa pande mbali mbali za dunia. Wote hao wanaonesha kuridhishwa kwao na dhamira ya dhati ya serikali safari hii kuwashirikisha katika ujenzi wa uchumi wao. Mfano mmoja ni Wanadiaspora wa Watanzania waishio Italia.
Uongozi wa Jumuiya ya Wanadiaspora wa Italia, umeniandikia kuniomba kushiriki kuandaa kongamano lao. Wamenieleza kuguswa kwao na utendaji wa serikali katika utekelezaji wa mipango yenye kulenga kuinua uchumi wa Watanzania wengi. Wanasema wanataka kufanya kongamano litakalohamasisha Watanzania waishio Italia kubaini fursa za uwekezaji zilizopo nyumbani na kuwavutia wawekezaji wa Italia kuja nchini.
Hakika, mwamko huu wa sasa Watanzania wanadiaspora unatokana na wanadiaspora kutafsiri kauli za watendaji wakuu wa serikali na kubaini dhamira ya kweli ya kauli hizo. Hivi karibuni lilifanyika kongamano la kujadili fursa za uwekezaji Tanzania nchini Sweden. Na katika kuonesha namna gani serikali hii inathamini mchango wa diaspora, si tu ilimtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga kushiriki, bali Televisheni ya Taifa, TBC, ilirusha moja kwa moja tukio hilo ambalo Dk Mahiga alikuwa mgeni rasmi wa kongamano.
Kama nilivyowahi kubainisha awali jambo hili lilikuwa halijapata kutokea huko nyuma. Wanadiaspora, nikiwemo, tumeingiwa na imani zaidi ya dhamira ya kweli ya Rais Magufuli ya kuongoza jitihahada za kuinua uchumi wa nchi. Watanzania kupitia matangazo ya TBC, tulimwona moja kwa moja Waziri Mahiga akielezea utayari wa serikali kuona uwezekano wa kuandaa taratibu za kisheria za kuwasaidia wanadiaspora bila kusubiri mabadiliko ya Katiba.
Kauli hiyo thabiti ya serikali ni faraja kubwa kwa Wanadiaspora na inawaongezea hamasa ya ushiriki wao kwenye ujenzi wa uchumi wa nchi. Hoja ya utayari wa Serikali kuweka taratibu wezeshi kwa diaspora kisheria ni mafanikio makubwa katika kuachana na mazoea ya nyuma ya mazungumzo matupu bila vitendo. Maana, baada ya miaka mingi ya nenda rudi kwenye ajenda ya uraia pacha, Wanadiaspora wameonyesha tayari na mpangilio ambao Serikali ya Awamu ya Tano inafikiria kuja nao.
Kwamba hata kama si kuwa na uraia pacha, basi, uwepo utaratibu wa kuwa ma Hadhi Maalumu kwa wanadiaspora walioko huko nje. Kwa kukumbushia na kuthibitisha dhamira ya serikali, hata kwenye uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri Mahiga alionesha ishara za serikali kulivalia njuga suala hili kwa kutambua mchango wa diaspora kwa uchumi wa nchi huku akiweka hadharani kila mwaka Sh trilioni moja zinaingizwa nchini na Wanadiaspora walio nje.
Katika hili, Wanadiaspora tunamhakikishia Waziri Mahiga na serikali kwa ujumla, kuwa siku serikali itakapowapa diaspora Hadhi Maalumu, haitasubiri muda mrefu kushuhudia trilioni hizo zikiongezeka kwa kasi kuja nchini. Tukumbushane dhana ya diaspora na maana yake. Neno diaspora lina chimbuko la lugha ya Kigiriki ikiwa na maana ya iliyotapakaa (enea).
Hivyo inapohusu jamii, ni pale raia wa nchi anapohama kutoka nchi aliyozaliwa na kuhamia nchi nyingine kwa sababu mbali mbali ikiwamo za kimasomo, kijamii au kiuchumi. Katika hili mtu anakuwa na sifa ya kuwa diaspora anapoishi ugenini kwa zaidi ya nusu mwaka. Moja ya tabia ya diaspora popote pale duniani ni kukumbuka nyumbani alikozaliwa. Kama wanadamu, tunakumbuka, mathalan, hata tulipokuwa wadogo, mara ile tulipoondoka nyumbani na kwenda kuishi kwa bibi au babu.
Hufika mahali, Diaspora tunakumbuka nyumbani kwa baba na mama. Kukumbuka ndugu wa kuzaliwa na marafiki tuliowaacha. Ikumbukwe, enzi za Mwalimu, mwaka ule wa 1985, Serikali ya Tanzania ilienda mbali zaidi na kuwa mfano wa kuigwa, kwa kuwapa Hadhi Maalumu Wajamaika Weusi (Rastafarians) waliotamani kurudi nyumbani Afrika. Hivyo, si wengi wenye kufahamu kuwa hoja ya diaspora na Hadhi Maalumu ina historia yake Tanzania. Desemba 12, 1985 Ofisi ya Rais, Ikulu ya Dar es Salaam ilitoa barua rasmi kuhusu ‘Waafrika walio ughaibuni’ hususan nchi za Magharibi.
Barua ilieleza kuwa Rais… “Agreed with principal of black africans returning to Africa.” Kwamba amekubali Waafrika weusi warudi Afrika. Barua hiyo iliwalenga hususan Wajamaika Weusi (Rastafarians). Barua hiyo ilisainiwa na Mizengo Kayanza Pinda aliyekuwa msaidizi wa Katibu wa Rais Nyerere wakati huo, Joseph Butiku.[/SIZE][/FONT]
[SIZE=5][FONT=times new roman]Hilo likawa jibu rasmi la serikali kwa maombi ya Rastafarians yaliyoanzia na mkutano wa Mwalimu Julius Nyerere na kiongozi wa Rastafarians Jah Mkhululi mwaka 1979. Taarifa hizi za kitafiti zimeandikwa na mwandishi mwanamama Monique Bedasse (Jah Kingdom, Rastafarians, Tanzania, And Pan Africanisim In The Rise Of Decolonization). Wanadiaspora tunamuunga mkono Rais wetu wa Awamu ya Tano kwa kuanza kwa vitendo kutambua na kuthamini mchango wa Wanadiaspora kwa kuchangia uchumi wa nchini, ikiwamo kuisukuma nchi kwenye kuelekea uchumi wa kati unajengwa na viwanda.[/FONT][/SIZE]

Aisee! Wanadiaspora msituyeyushe, rudini nchini tuzisome wote namba…

Pumbavu sana, unajifanya hujui tunavyoteseka