Mwanamke afariki akiongezwa ukubwa wa maziwa Kenya

[ATTACH=full]176086[/ATTACH]

Bodi ya madaktari nchini Kenya imeitaja zahanati ambayo mwanamke mmoja alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa yake kabla ya kufariki, kwa mujibu wa gazeti la nchini Kenya la Daily Nation. Afisa mkuu wa bodi hiyo Daniel Yumbya amesema ni zahanati ya Surgeoderm Healthcare iliyo Nairobi, iliohusika na kisa hicho kilichosababisha cha Bi June Wanza wiki iliyopita.

Bw Yumbya alisema bodi hiyo ilikuwa imeiandikia zahanati hiyo kutaka ieleze sababu zilizosababisha mwanamke huyo alazwe kwenye hospitali ya Nairobi ambapo alifariki. Pia imeomba ripoti kutoka kwa Hospitali ya Nairobi. Zahanati hiyo iliyo barabara ya Thata mtaa wa Kilimani mjini Nairobi imeweka matangazo kwenye mtandao wake kuelezea huduma inazotoa ukiwemo upasuaji huo wa kuongeza au kupunguza maziwa.

Bi Wanza alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa yake lakini akakumbwa na matatizo ya kiafya. Kisha alienda kutafuta usaidizi wa matibabu kwenye hospitali ya Nairobi siku ya Jumatano kabla ya kufariki siku ya Alhamisi wiki iliyopita. Gazeti la Daily Nation lilisema kuwa madaktari walijaribu kumuokoa Bi Wanza baada ya kugundua kuwa sehemu ya utumbo wake ilikuwa imekatwa kufuatia upasuaji huo.

Source: BBC

Wanahangaika nini kwani?

Du! Sio mchezo wanawake wanapenda sana kuhatarisha maisha yao

Tatizo sio wanawake. Tatizo ni sisi wanaume. Tunapenda saana milima ya matiti.

Kazi wanayo,yaani wanatutafuta at any cost…

Inasikitisha sana…

Mambo hayo wanaweza zaidi Marekani…

Cc: @Mahondaw

Maziwa bhana

Yule wa TZ dada wa Juu anasEMA kakatwa utumbo.

Dunia inatupelela kasi, yote iyo uridhishe watazamaji

Tatizo wanaume nyie jmn!!

Urembo,fasheni na wanaume wanawapeleka puta wanawake…ipo sikj watasema wanataka muwe na mapengo daah mking’oa ndio jumla hiyo

Duhh kuna watu wana hatari acha nibaki na saa 14 yangu

Iwe funzo katika jamii

Kama zile enzi za mwanya, kuna watu hivi sasa wanatisha

Kapoteza uhai kisa kurekebisha maumbile aliyoumbwa na God

Ni upuuzi uliopindukia kwa mwanamke kubadilisha maumbile ili tu awaridhishe wanaume

kweli tunatofautiana, hv kuna wanaopenda maziwa makubwa? Hv wanawake wanawake wanapovaa nguo fup, kujibinu na mambo mengne meng kama hayo lengo lao n kuwaringshia wanawake wenzao au kuwatamanisha wanaume au vyote, kipi hasa? Nataman sana kupata majib