Mwenda Tezi na Omo Marejeo ni Ngamani

Nimevuma,nimekwima,
Nimepaa,nimeelea,
Nimeabiri,nimesafiri,
Nimetambaa,nimetembea,
Nimeenda Tezi,nikafika Omo;
Nimerejea Ngamani.……kijijini.

Sasa nenda mmnn huku ni graveyard of memories

navy seal pia nimeland

Karibu sana mwalimu. Tulikukosa sana.

Mwalim @xuma nyorosha hichi kisweli
Makosa imefanyika

village idler muzeeee niaje

Hajafuma mbali.

Bora usilijue usilolijua kuliko kulijua usilopaswa kulijua

Haiyumkini umesafiri miaka dahari kuyafuata ya hatari

Lakini safari hufunza kwa kila anayetaka kujifunza

Mja akirudi atokako kiungwana hayo ni mawaidha mema atufundisha

Karibu sana mgeni mwenyeji.

Ndimi pangu pakavu
@Baba yake Digi

Alamsiki

Omo nimemaliza. Siku hizi natumianga sabuni ya kipande.

7th handle n kicking… Mbona admin hajibu maswali tukifungiwa password?

@xuma wacha stori za Omo,Arial ina guarantee right now. But that’s not the point.
Ulikuwa wapi? Why did you leave? Were you here under disguise? Why have you come back? Are you expecting we lay out the welcome mats or what? Apart from the kisweli,umeleta nini?

Hehehehe! Niliondoka kutafuta malisho mabichi kaka.
Mimi ni mwenyewe katika asili ya mtu na utu; siigi wala sijifichi,ila tu jina langu sawia lako ni la Majazi!
Nimerejea kuendeleza nilicho na ninacho kienzi…kiswahili/Lingala,
Mwendo wangu si was vishindo bali wa kunyapianyapia…zulia (carpet and not mat) zilihitaji kwa sasa babu @le scumbag!!

Bobea,bobea,bobea.
Tulikuwepo,tukateka,tukavuma,tukakwima …mti mle!!

Hehehe! Mnyambuliko wa vitenzi hapa umekandamizwa.

Swadakta
Waweza nipa yaliyo kificho, pengine naweza kuwa na jibu

Thiì na kùu…

tuitie simiti,njia upitayo?
Au tukuwekee na kiti,uzidi pumbao
Huko Omo na tezini,wenye gharika kunao?
Alorudi ngamani,hurudia mafao
Mbuzi alokufa supuni,hajafia kwao.
Karibu jumbe amani,tuchangie hiki kikao.

Hehehee.

Learnt something new Tezi - Nyuma /Omo - Mbele/Ngamani - Katikati

https://news.un.org/sw/audio/2018/05/1016761

Kutokana na sehemu za meli.