MWENDESHA MTUMBWI POPOTE ULIPO

SIJUI KAMA MWENDESHA MTUMBWI ANAKUMBUKWA

PICHA NA ELIMU KUBWA na Michael S. Mbiti Jr. Anatililika

Picha hii ni ya mwaka 2010, yaani miaka nane iliyopita. Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu).

Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huo, Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.

Miaka mitano iliyofuata Majaliwa akawa Waziri Mkuu. Ukiangalia picha hii unapata jawabu kuwa hakuna ambaye alikuwa anawaza kama Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Mizengo Pinda.

Hapo Majaliwa alikuwa akionekana mwenye cheo kidogo tu, Mkuu wa Wilaya. Pichani anaonekana ni mtu mnyonge tu, mnyeneyekevu mbele ya wezake.

Majaliwa wa leo huwezi kumpandisha kwenye mtumbwi hivyo, maana ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika ofisi yake kuna kila aina ya usafiri bora ambao unaweza kumfikisha popote, tofauti na mtumbwi huo ambao unaona kuupanda ni kama vile kuhatarisha maisha.

Majaliwa ana ndege yake kama Waziri Mkuu, ana helikopta na magari. Majaliwa wa leo hawezi kuvuka Mto Rufiji kwa mtumbwi hivyo, helikopta itamvusha.

POKEA ELIMU HII

Mwenye kibali cha kuyafahamu maisha yanayofuata kwa kila binadamu ni Mungu tu. Mungu alijua Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Pinda, ila watu wengine wote kwenye mtumbwi huo akiwemo nahodha na Majaliwa mwenyewe hakuna aliyeifahamu siri hiyo.

Picha hii inafundisha watu kuwa wanyenyekevu katika maisha yao. Unaweza kumdharau mmachinga anayekubembeleza kununua bidhaa zake lakini miaka inayofuata ndiyo akawa Rais.

Ukijiona umebarikiwa kwa maisha fulani usiongeze tambo, bali mshukuru Mungu na uwe mnyenyekevu. Unaweza kumdharau housegirl nyumbani kwako, baadaye akawa Rais mwanamke au mke wa Rais, na mkamwita First Lady kisha barabarani mkapanga foleni kwa kuzuiwa na traffic, maana First Lady anapita.

Si mnasema kupanga ni kuchagua? Basi mpangaji ni Mungu na yeye ndiye humchagua amtakaye. Anaweza kumchagua kumwinua mtu ambaye wewe unamchukia kupita kiasi, acha chuki. Anaweza kumchagua unayemdharau, hebu acha dharau. Anaweza kumchagua unayemwonea na kumnyanyasa kwa unyonge wake, tafadhali usionee wenzako.

Ishi maisha ambayo yatakufanya uwe huru leo na kesho. Tenda wema na kama huwezi basi usitende ubaya. Usipomtendea mtu ubaya utakuwa huru kila siku. Na utatabasamu kwa mafanikio ya kila mmoja. Ukiwa mwovu, kuna watu wakifanikiwa utaona wanaifanya dunia yako iwe chungu.

Tafakuri.

Brother Katelephone is a humble guy.

Sana

Ni kweli kabisa…

Tatizo binadamu ni wabishi sana…

Cc: @Mahondaw

uko sahihi

Safi kabisa elimu nzuri

Haaaaahaaaaaaa

safi, kuweni na amani na watu wote!

kama kuna tatizo ita kirafiki unapata mawazo yake kirafiki tu…mbona mambo yataenda tu kipoa poa tu…

Ha ha haa… :D:D:D

Watu wa Pwani hawanaga visokolokwinyo.