Niko na mshangao…
Hadi sasa bado sielewi elewi tuu, kuna mtu kanisukuma kuingia humu sasa bado hata sielewi na utu uzima tuu naona wakati unaniacha nyuma.
Kwanza kuanzisha uzi mpya hapa nimeotea tuu hata sijui kama utatokea au ntakuwa nachangia uzi wa mtu, sijui kama ntaweza aiseeh.
Hata jinsi nilivoingia humu Kasie mie hata sielewi elewi…
Basi wakati JF ikiwa imefungwa nikaanza kusoma vitu vingine mbalimbali badala ya kupiga soga. Hapa ndo nikajijua kuwa kumbe Kasie niko hivi…
Top definition
Kasie
Kasie is wonderful!
-hilarious
-very sexy
-incredible wife
-some may even call her superwoman
-has some peculiar children
-great eye-candy
-good dancer
-gets no cheese on sandwiches
-likes a nice waltz
-not fond of football games
Kasie, being superwoman, loves superman.
#awesome#interesting#phemomenal#comical#personable
by chica misteriosa December 12, 2010
Hiyo tafsiri nimeikuta huko Urban Dictionery… hivi kumbe Kasie mie ni Super Woman… hata sikuwa najua yeeey am happy for that.
Ila ndo hivyo, huku badla ya kuitwa New Member naona nimepewa utambulisho wa New Villager… ati mie ni Mwanakijiji…
Kasie Mahaba Matata.
Siku moja tu kwangu ni mwaka nilipata mawazo sana juu yako mkuu na thread zako
Mwifwa
4
Jitahidi upande nagzi uitwe Mwenyekiti wa nyumba kumi
Mpaka sasa sijaamini, Team Jf tumehamia huku kenya Talk.
Huu mtandao nimejiunga siku nyingi Sema nilikuwa sikielewi kiswahili cha hawa Jirani zetu.
Mwifwa
7
Mimi pia tangu March nipo humu ila kiswahili chao ndio ilikuwa changamoto
Huku wote ni villager haijalishi unaishi city centre au kakonko
Sasa Angalau najihisi sasa Nipo Nyumbani.
We Kasie una mbwembwe kweli haya karibu New villager mwenzangu
Hhahahahahaha naona wewe ni Kiongozi wa Kijiji sijui ndo Chifu…!!! hahahahahaa
Haya wacha nijikongoje nifikie huko. Naona saa hizi nimekuwa Mwanakijiji kamili.
_255in
16
Siku ile nilikupa ofa ukakimbia…
Hata mie bado nashangaa shangaa… kumbe thread imekubali.
Hhahahahahhaa nimeipenda hiii, kuwa huku wote tunakuwa wanakijiji haijalishi unakaa Daslam au Kondoa au USA Baby… hehehehehheee
Ngoja anisikie namsema huku USA Baby akija nakimbia mbiooo.
Hhaahahhahahaaa abee Kim. nna mbwembwe gani jamanii, mbona niko mpole tuu hheheheheee
Ila mwenzio sasa hivi nshakuwa mwanakijiji kamili sio mgeni tena. Pambana ndugu yangu.