NAOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI KENYA.

Ndugu zangu wakenya mimi ndugu yenu nakuja mbele yenu nikiomba hifadhi nchini mwenu maana Bongo hakueleweki sasa. Nimemaliza chuo kazi hakuna, Nimetembea na bahasha miaka mi4 bila mafanikio, Unatembea na bahasha mpaka inabadilika rangi ilikuwa ya kaki inakuwa nyeupe. Ukifungua genge la nyanya TRA wanakuja, Genge la mtaji wa laki 2 wanakudai kodi Laki1 ulipe kila robo ya mwaka. Mtaani watu hawana hela kila mtu analia ukata ukimuoma mtu mia5 anakwambia usubiri kidogo kuna watu anawadai wakimlipa atakupa. Ukiwa msanii unafungiwa nyimbo, ukilima mahindi hasara kilo sh200, choroko, kunde kilo sh100, ukivua samaki unakamatwa, ukiwa mgahawani unakula samaki wanakuja na rula kupima samaki akiwa mdogo unakamatwa. ukifungua blog au website kibiashara inafungwa. vikwazo vya vijana kufanikiwa bongo leo ni vingi mno. kijana kuwa milionea bongo sasa ni ndoto. So kama hamtajali naombeni hifadhi ya muda huko nije nitafutie maisha huko.
Asanteni
Risk.

kambi ya wakimbizi ya kakuma iko uko>>>>>>>>>

https://www.kenyatalk.com/index.php?forums/tanzania_talk/

Hakimoto sijakuelewa mzee

Pole sana…

Hayo yote ni maisha, ipo siku yatakiwsha…

Cc: @Mahondaw

Pole sana mkuu, vumilia hii ndio bongo usipokomaa nani ataibadili?

Matatizo katika nchi za Kiafrica hufanana bora utafute chaka bara jingine

Thanks wadau

Natamani kwenda mabara mengine chief but how do i reach there bila hela na watu ninaowafahamu

Kama pesa hakuna kweli itakua ngumu basi anza Kenya utajikuta unazidi kupiga hatua

Hahahahahahah

Angalia, ya Kenya yakikushinda usije ukajikuta upo Somalia…

Hukupata kusikia ya kuwa ni heri yule alalae chini nyumbani mwa babae kuliko yule mtumwa kwenye nchi ya waajemi?

tuungane tu …hifadhi hata Somalia poa tu

Naona hii nchi nayo inaelekea kuwa somalia nyingine, kama watu tunapangiwa mavazi, mambo ya kupost, muda wa kulala, muziki wa kusikiliza na n.k unategemea nini!

Una akili timamu kweli?

Unaongea na musiba au unaongea na jiwe!!

Wakenya wenyewe ni wakimbizi hapa Tanzania

Kambi yao ipo maeneo gani