NAOMBA KUELIMISHWA KUHUSU HII SHERIA YA USAJILI WA BLOGS TANZANIA

Mimi kama mmoja wa wadau wakubwa wa mtandao wa Jamii forums (ingawa situmii jina hili kule) nimeadhirika kwa kiasi kikubwa kwa Jamii forums kufungwa.

Jamii forums imekua na faida nyingi sana kwetu sisi kama wadau, Pamoja na kutoa elimu na kuhabarishana nina ushahidi kwa wadau wengi kupata msaada wa kazi au matibabu kwa wataalamu wengi waliopo kwenye Jamvi lile.

Sasa hichi kipengele kwenye sheria ya usajili wa blogs kwamba member atambulike ndio inakuweje, Ina maana hawa Jamii forums ndio wawe na taarifa zangu halisi wakati najisajili lazima niwapae nakali ya kitambulisho/passport/leseni ya udereva au nyaraka yoyote ya kunitambulisha mimi.

sasa kule kuna raia wapo serikali lakini kwakua hawatambuliki wanaanika uozo wa serikali, ina maana hii hawa jama tutwakosa kuna waliopo ccm chadema na Cuf wanatumia ila hali yakua anonymous kuanika mauvu ya vyama vyao.

Naombeni kujuzwa na wanaolewa.

Mkuu,hii sheria ilitulenga sisi(JF).

Wanataka mtu ajisajili kwa utambulisho halisi.

WTF.

Bwahahahahaaaa They are not serious aisee.

Ni kweli kabisa ilitulenga JF maana ndio jukwaa pekee lililokuwa linaibua kina aina ya Maovu kwa kila mmoja hasa walioko serikalini.

Mbali na hivyo JF ilikuwa na msaada sana kwa serikali japo ndio wanaipiga vita hatimaye leo ipo mikononi mwao.

Nimetembela Forum mbalimbali kubwa Duniani ikiwemo Skyscrapercity Forum, watu wamejisajili kwa majina fake.

Hamna sheria inayokataza watu kujisajili kwa majina fake isipokuwa ni figisu tu za huu utawala ambao hautaki kuambiwa ukweli na kukosolewa.

kikwete tunakukumbuka baba!! acha tuendelee kuisoma namba, mbele kwa mbele kabisa daahhhh…twafa!!

Ujinga tu.
Wajifunze kwa wenzao.

Twafah

@pumbu wewe ulikuwepo JF kweli? Hayo Majina kule JF ni noma

HAta mimi binafsi nimeathirika pakubwa. Ilikuwa ni sehemu ya kubadilishana mawazo, kuelimisha, kufahamishana na burudani kwa ujumla. Ila kama mtu atapaswa kutoa taarifa zake zote ndiposa asajiliwe kwenye mtandao wa kijamii, mbona wengi watakoma! Ila naona JF ndio walikuwa walengwa na sheria hizi kandamizi…

nipo mda tu mkuu… kiboko wa ‘ze nyumbuzz’ kule… #planet pumbunyo si unajua tena

Huyu si ndo alimkata mamvi?

Malaika mkuu hataki kukosolewa, aliomba Malaika washuke wafunge mitandao nadhani sasa imefika mahala pake. Hata hivyo ni wabunge wa ccm walipitisha sheria hii kandamizi ambayo inawathiri wenyewe

https://2.bp.blogspot.com/-uPS0WlEgHuI/Wx-puoDYDcI/AAAAAAAB8Hc/3BSC4U-wQ38eCpvztt-0Al7B6kLIT0T-wCLcBGAs/s1600/1.JPG
Sakata la Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutekeleza kanuni za maudhui, limewasilishwa bungeni na mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea akitaka maelezo ya kina ya Serikali kwani inaminya uhuru wa habari.

Kubenea akitumia Kanuni ya 47 (1) (2) (3) leo bungeni Juni 12, 2018 akitaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili suala hilo.

“Kuanzia jana TCRA imesitisha usambazaji wa taarifa za social media, kwa tangazo hilo YouTube zote haziruhusiwi toka jana, Blog zote haziruhusiwi toka jana, website na redio zote ambazo ziko online haziruhusiwi toka jana,” amesema Kubenea na kuongeza:

“Kwa hiyo Mamlaka ya Mawasiliano wanasema mpaka Juni 15 mwaka huu, wale ambao watakuwa hawajalipia ada zao hawataruhusiwa. Mahakama Kuu kanda ya Mtwara ilisitisha hivyo nao wakazingatia agizo hilo la Mahakama.”

Kubenea amesema, “jana asubuhi, tangazo linatoka na watu hawajajiandaa, Bunge liahirishe shughuli zake za muda ili mjadala huu lijadiliwe na Serikali iweze kujibu suala hili, dunia imesimama hakuna taarifa zinatoka Tanzania kwenda kwingine na hata webstite zingine za serikali hazitoki nje.”

Akitoa maelezo ya kiti, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesema, “hili la Kubenea sisi bungeni hatuwezi kuahirisha, waliofunga wana sababu zao na watakapokuwa tayari watafungua kama kawaida.”

Wanapenda kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.
Washezi tu hao

Hizi sheria za kujulikana kwenye forums ni kuna watu wanatafutwa kwa kuanika uovu wa mambo yanayoendelea…

Kinachowaumiza vichwa ni ile hali ya mipango ya hovyo inafanyika kwa siri, lakini baada ya muda mchache unakuta taarifa zote zipo JamiiForums…

Cc: @Mahondaw