Mimi kama mmoja wa wadau wakubwa wa mtandao wa Jamii forums (ingawa situmii jina hili kule) nimeadhirika kwa kiasi kikubwa kwa Jamii forums kufungwa.
Jamii forums imekua na faida nyingi sana kwetu sisi kama wadau, Pamoja na kutoa elimu na kuhabarishana nina ushahidi kwa wadau wengi kupata msaada wa kazi au matibabu kwa wataalamu wengi waliopo kwenye Jamvi lile.
Sasa hichi kipengele kwenye sheria ya usajili wa blogs kwamba member atambulike ndio inakuweje, Ina maana hawa Jamii forums ndio wawe na taarifa zangu halisi wakati najisajili lazima niwapae nakali ya kitambulisho/passport/leseni ya udereva au nyaraka yoyote ya kunitambulisha mimi.
sasa kule kuna raia wapo serikali lakini kwakua hawatambuliki wanaanika uozo wa serikali, ina maana hii hawa jama tutwakosa kuna waliopo ccm chadema na Cuf wanatumia ila hali yakua anonymous kuanika mauvu ya vyama vyao.
HAta mimi binafsi nimeathirika pakubwa. Ilikuwa ni sehemu ya kubadilishana mawazo, kuelimisha, kufahamishana na burudani kwa ujumla. Ila kama mtu atapaswa kutoa taarifa zake zote ndiposa asajiliwe kwenye mtandao wa kijamii, mbona wengi watakoma! Ila naona JF ndio walikuwa walengwa na sheria hizi kandamizi…
Malaika mkuu hataki kukosolewa, aliomba Malaika washuke wafunge mitandao nadhani sasa imefika mahala pake. Hata hivyo ni wabunge wa ccm walipitisha sheria hii kandamizi ambayo inawathiri wenyewe
Kubenea akitumia Kanuni ya 47 (1) (2) (3) leo bungeni Juni 12, 2018 akitaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili suala hilo.
“Kuanzia jana TCRA imesitisha usambazaji wa taarifa za social media, kwa tangazo hilo YouTube zote haziruhusiwi toka jana, Blog zote haziruhusiwi toka jana, website na redio zote ambazo ziko online haziruhusiwi toka jana,” amesema Kubenea na kuongeza:
“Kwa hiyo Mamlaka ya Mawasiliano wanasema mpaka Juni 15 mwaka huu, wale ambao watakuwa hawajalipia ada zao hawataruhusiwa. Mahakama Kuu kanda ya Mtwara ilisitisha hivyo nao wakazingatia agizo hilo la Mahakama.”
Kubenea amesema, “jana asubuhi, tangazo linatoka na watu hawajajiandaa, Bunge liahirishe shughuli zake za muda ili mjadala huu lijadiliwe na Serikali iweze kujibu suala hili, dunia imesimama hakuna taarifa zinatoka Tanzania kwenda kwingine na hata webstite zingine za serikali hazitoki nje.”
Akitoa maelezo ya kiti, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga amesema, “hili la Kubenea sisi bungeni hatuwezi kuahirisha, waliofunga wana sababu zao na watakapokuwa tayari watafungua kama kawaida.”