Naomba Msaada Wandugu.....

…naomba mtu alieona (au kusikia) taarifa ya habari ya ITV leo hii jioni anithibitishie hiki nilichokiona leo kuwa ni kweli NIMEKIONA NA KUKISIKIA.

Waziri wa ujenzi na uchukuzi Issack Kamwelwe (naona aibu kumuita Engineer kama anavyopenda aitwe - na jinsi wengine humuita) ametoa amri kwa ATCL kuhakikisha kuna dirisha lao la kukatisha tiketi za ndege za ATCL kwenye kila kiwanja cha ndege. Hilo (kama ndilo aliloagiza) halinipi shida hata ikiwa ATCL watatekeleza agizo lake hilo Lake Manyara. Ila kuna agizo alilotoa kuwa anahitaji maelezo ni kwa nini bei ya tiketi za ndege zinakuwa juu pale mtu anapokuja kutaka tickets dakika za mwishoni kabla ya safari!!!
Naomba msaada ili nipate uelewa.

Hmm! habari hii sijaisikia, ngoja nifanye utafiti mdogo… Na kama ni kweli, basi itabidi tutafute huyu Kamwelwe ni injinia wa nini!..

Isaac Kamwele ni Civil Engineer Mkuu.

Hmm! Sishangai maana ukishaingia kwenye siasa unaweza kufanya au kusema lolote hata lisiloendana na taaluma yako…

Ana vyeti vinavyomtambulisha kuwa ni civil engineer lakini sidhani kuwa ana competence anayopaswa kuwa nayo civil engineer.

Hakuongea kama injinia bali ameongea kama mwanasiasa

Mkuu wewe ni mgeni nchi hii?

Navyojua mimi…

Kuna high season ticket zinakua juu na kuna low season ticket zinakua bei ya kawaida…

Kuna safari za usiku wa manane ticket zinakua cheap, kuna safari za kutwa ticket zinakua bei juu…

Kuna kukata ticket siku kadhaa nyuma kabla ya safari yako, kuna discount unapata, kuna kukata ticket last minutes bei inakua bila discount ndiyo pale unapohisi bei imekua juu sana, mbona fulani alikata mwezi uliopita ilikua cheap mimi nakata leo leo bei inakua juu…

Cc: @Mahondaw

Good observation. Sasa inakuwaje waziri mwenye dhamana ya usafirishaji (na engineer wa kusomea) asijue kitu basic hivi? Ata-formulate policy gani itakayowezesha mazingira bora kwenye sekta ya usafirishaji?

Tupo zaidi kwenye kukusanya mapato… hatuna akili ya kucheza na nyakati za biashara kuvutia wateja…

Cc: @Mahondaw