Naomba msaada wenu wakuu

Salaam kwenu wapenzi wa jukwaa hili.

Naomba kwa yoyote aliye na Business proposal ya kuanzisha kiwanda kidogo cha kukamua Alzeti anisaidie maana hali inazidi kuwa mbaya. Nimejaribu kupambana na hali yangu lakini naona dalili zote za kushindwa katika maisha haya, na katika pita pita zangu nikakutana na mtu akaniambia nije na proposal ili aone jinsi ya kuokoa jahazi.

Nawasilisha kwenu wakuu

Una shilingi ngapi, maana kuandaa proposal si kazi ndogo atiā€¦

Una shilingi ngapi nikuandalie?

Duh mwenzenu analalamika hali mbaya na anaomba msaada ila bado tu watu mnataka kumkamua mkwanja

Fursa hiyo. Watu lazima waitumie

Hapa ni full kukamuana. Mbaya saaaaana

Andaa pesa kwanza proposal ni hela

Aisee!

Ndiyo asili yetu watanzania ndugu, pesa mbele bila kujua kwamba unaweza kumsaidia mtu halafu in return ukafaidika zaidi ya pesa uliyokuwa umetanguliza mbele

Ingiza mtandaoni utapata samples nyingi za zenye kufanana fanana na hitaji lako, chagua moja uimodify ilingane na matakwa yako.

Hii kupenda vya bure ndio maana watanzania hatutaendelea. Kuandaa hiyo kitu ni taaluma za watu. Maisha ni kutegemeana

Nimepata mkuu, Shukrani sana

Pitia JF kuna Nyuzi kibao mle za kuanzisha proposal kwenye Jukwaa la Uchumi na Ujasiliamali.

Shukran

Shukran sana mkuu

Naona kufa kufaana