Nchi maskini kama tz,ke,ug n.k zinaweza kujitegemea bila kuomba misaada wazungu? Jibu ni No!!

Changamoto iliyopo kwenye nchi nyingi za kimaskini ni kuwa na kitu kinachofahamika kama “budget deficit” karibia kila mwaka, hii inatokana na kuwa na matumizi mengi kuliko uwezo wa nchi wa kuzalisha mapato. Fikiria kwa mfano malipo ya mishahara ya walimu nchi nzima, manesi na watumishi wote wa serikali hapo wote wanataka mishahara yao iflow kama kawaida kila mwezi. Jenga picha kama serikali yenyewe ndio ingesimamia utoaji wa Huduma muhimu za Bure Kama ununuzi wa madawa ya ARV na matibabu ya Ukimwi na TB kwa RAIA wake serikali zetu hizi zingehimili huo mziki? Mapato ya nchi kuongezeka yapo limited to the way serikali husika inavyofanya " good reallocation of human resources, capital resources and financial resources" lakini kinyume na hapo tutaendelea kuona nchi zetu hizi zikimpigia magoti Mzungu. Na mpaka lini nchi zetu hizi zitaendelea kuwategea wazungu wawape misaada kwa ajili ya maendeleo yao? Na ni nini tatizo kwa sisi ngozi nyeusi kushindwa kuliweka bara hili salama mbona kabla hatujapewa post za kuwa watawala huwa tunatoa maelezo mazuri ya namna ya kuongoza nchi zetu nini hutubadilisha mpaka kujikuta tumesahau zile harakati zetu za kulikomboa bara hili? Mfano mkuu wa kaya ya tz kipindi akiwa mbunge alionekana anatetea sana maslahi ya nchi lakini baada ya kupewa urais deni la Taifa linazidi kupaa kwenda juu nini tatizo? Je kwa muendelezo Huu wa kuomba misaada wazungu je tutapona kweli dhidi mikono michafu ya mabeberu? Misaada kutoka kwa wazungu haiji Bure inaambatana na Masharti magumu ikiwemo kuwakabidhi baadhi ya rasilimali zako muhimu kama ardhi yenye madini au rutuba. Kwa namna dunia ilivyo draftiwa na mabeberu(wazungu) vitu muhimu kama Technojia kumilikiwa na wao tutegemee nchi maskini kila mwaka kuwapigia magoti wazungu wawape misaada. Kujinasua kutoka kwenye utegemezi huo labda mpaka Yesu arudi.

Mzungu katutangulia tayari tena miles, itachukua decade kumpata ila tutampata tu mana we have each and everything, Marekani alikuwa under great britian ila now tunaona alipo

Tunasikitisha sana…

Tukipata katiba itakayoweka mambo yote wazi na kwa muongozo mzuri… mgawanyo mzuri wa nguvu za madaraka bila kuingiliana kwenye maamuzi… kutokutegemea ukusanyaji pekee wa kodi kitu ambacho inatulazima kutoza kodi hata kwenye mambo yasiyostahili ili mradi pesa ipatikane hatimae kuvuruga uchumi na maendeleo kusuasua au kuchelewa au kutokuwepo kabisa…

Cc: @Mahondaw

Nchi hizi zikiweka mazinngira mazuri(Mazuri sana) kwa private sector kukua na wakiweza kudhibiti ubadhirifu serikalini hata kwa kiwango cha jiwe tutatoka.

Jiwe kajitahidi suala moja ila anatakiwa ajifunze jinsi Sumsung, Hyundai , LG nk yamekuwa makampuni makubwa.

Ufisadi,majivuno,uzandiki,tamaa,ubinafsi, Ndio kinachozidi kuturudisha nyuma badala ya kusonga mbele

Hatuwezi kutoka kwa style hii ya mambo yanakwenda bila bajeti?! Mtu anasema tu chukua bilioni kumi peleka kule !!!huyo waziri a fedha ndio zigo linamuangukia ila hana jinsi!!miradi iliyowekwa kwenye bajeti na pesa yake kutengwa inakosa pesa ,miradi mipya ambayo imeibuka tu from no where ndio inapata pesa ?!!kingine una kopa mikopo ya kibiashara kujengea miradi ambayo faida yake utaanza kuipata baada ya miaka 15!!huku hiyo mikopo unapewa grace period ya miezi mitatu tu kuanza kuilipa!!kinachofanyika sasa inabidi pesa ya kuanza kuhudumia mkopo huo uzichukue kutoka sehemu nyingine kuna nini hapo???!!wakati kuna mikopo ya aina hiyo ya miradi utaanza kuilipa mala tu mradi utakapoanza kufanya kazi!!!KWELI #MKUKI KWAO POLINI

Your sick view is absolutely laughable to the genuine intelligent people.dont waste your darling time on such disgusting conclusion.

You are just the same, 'cause you are judging/ criticizing him instead of helping him become intelligent as you said…

Kujitegemea ni ndoto hata Mkulu huwa anaiota sana

impossible hasa kwa mipango hii ya kudanganyana ili mtu upate sifa kwa wananchi, takwimu zinapindishwa ili kupata sifa siasa, uwazi katika mambo ya kiuchumi hayapo mf mapato ya wizara anayajua rais na wazir wake Kairuki na hayatakiwi kuwa questionable, upigaji ule ule tofauti ni zama tu

In the long term zinaweza kujitegemea wananchi wake wakijituma kufanya kazi kwa maarifa na weledi… Tukiamua kuacha kupenda mteremko itatuchukua kama miongo miwili hivi…sio ngonjera za Serikali ya ccm kipindi kile baada ya kunyimwa msaada hapo hapo wakasema tunaeza kujitegemea

Tunaweza toka lakini sio leo wala kesho. Inatia hasira kuona bango kubwa Tohara kwa msaada wa watu wa marekani!!! Kama kutahiriwa tu tunategemea misaa ya marekani mengine tutaweza?
Au utamsikia kiongozi mkubwa tu anafungua jengo la mafunzo ya kijeshi, eti Tunawashukuru ndugu zetu na rafiki zetu wa China kwa ufadhiri huu!! Sura kavu hata soni haoni, toka lini mzungu au mchina akawa rafiki yako?