Ndoa siyo group la whatsapp

#1
Dada ambaye hujaolewa na unapenda maisha ya ndoa, elewa kuwa ndoa siyo group la whatsapp au facebook, ndoa siyo jumuia, ndoa siyo zawadi kwa wazazi, ndoa siyo social status, ndoa siyo watoto, ndoa siyo kuondoa nuksi:

1. Usiolewe sababu eti rafiki zako wote wameolewa
2. Usiolewe sababu eti ‘classmates’ wako wote wameolewa na wana watoto
3. Usiolewe sababu eti umemaliza chuo, unaishi mwenyewe na una kazi nzuri
4. Usiolewe sababu eti kila mtu kanisani anakuuliza pilau tutakula lini
5. Usiolewe sababu eti wazazi wanataka kumuona mkwe na wajukuu
6. Usiolewe sababu eti umechoka kuchangia wengine sasa unataka kuchangiwa
7. Usiolewe ili eti uonekane umeolewa (wenyewe mnaita kutoa mkosi)
8. Usiolewe sababu eti umepata ujauzito
9. Usiolewe sababu eti unaogopa kuzeeka ukiwa mwenyewe
10. Usiolewe sababu eti unaona umri unakwenda

Olewa kwa sababu ni wakati ambao Mungu kakupangia kuolewa, umempata mtu sahihi mnayependana kwa dhati, na umeridhia kutoka moyoni bila kushawishiwa. Vinginevyo endelea kuishi mwenyewe kuliko kuingia kwenye ndoa ya majuto…
 

Top