Nitaendelea kuwa ' Neutral ' Kimtizamo, Kimawazo, Kifikra na Kimaudhui hata huku

[FONT=courier new]Imenibidi tu nije na hili ’ bandiko ’ muhimu hasa baada ya Watu fulani fulani kunifuata PM huku wengine wakinipongeza wakidhani kuwa nipo upande Wao na wengine pia wakinilaumu kwa kudhani kwamba labda nina ’ chuki ’ nao au ’ Uadui ’ nao au natumika kwa maslahi ya Watu fulani.

[COLOR=rgb(184, 49, 47)]UFAFANUZI na MSIMAMO wa GENTAMYCINE hapa Jamvini na kokote nitakapokuwa ni…

Najua na nakiri tena hapa kwamba Mimi ni mwana CCM ( japo sina Kadi yoyote ile ) ya Chama ila ni Chama ambacho nimetokea Kukipenda na isitoshe nimekikuta na sioni aibu pia kusema kwamba kwa namna moja au nyingine pia ni Chama ambacho ’ kimenikuza ’ vile vile kulingana na ’ historia ’ yangu ya Kimaisha.

Kiasili ( naturally ) kabisa Mimi ni Mtu ambaye huwa napenda sana kuwa ’ neutral ’ katika mawazo na misingi yangu ya ’ Kifikra ’ hasa hasa katika mambo yahusuyo Siasa na Uongozi unaojumuisha ’ Utawala ’ wa Tanzania. Huwa sipendi kuona Mtu fulani anakosea / anakengeuka au labda Watu fulani wananyimwa haki zao kwa ajili tu ya ’ Umangimeza ’ wa ama Mtu fulani au Watu fulani.

Niliwahi kusema kule JamiiForums na leo narudia tena kuliweka hili wazi kwamba japo Mimi ni ’ Mshabiki ’ tena ’ Kindakindaki ’ kabisa wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) ila pia ni ’ Mshabiki ’ wa Vyama vya Upinzani hasa vile ambavyo naona kabisa kwamba vinaleta tija Kidemokrasia na pia vinaipa ’ Changamoto ’ CCM ( Chama Dola ) katika kufanya vyema.

GENTAMYCINE siku zote nitakuwa wa Kwanza Kuwapongeza au Kuwakosoa wana CCM pamoja na Serikali yake bila aibu au upendeleo lakini GENTAMYCINE huyu huyu tena nitakuwa wa Kwanza Kuwakosoa au Kuwapongeza ’ Wapinzani ’ wa Tanzania bila hofu wala haya yote ikiwa ni katika muendelezo wangu ule ule wa kuwa ’ Neutral ’ katika yale yote ambayo nayaamini, nayakubali na nayaona yako sawa.

[COLOR=rgb(184, 49, 47)]KUWASEMA TCRA haimaanishi nawasema SERIKALI 100%

Ni kweli kabisa kama kuna Mtu ambaye aliumia na mpaka leo bado naumia hadi kusikitika kwa Mtandao wangu ’ pendwa ’ wa JamiiForums kutokuwepo hewani basi ni Mimi GENTAMYCINE na wala hapa sipepesi macho, sitikisi masikio wala simung’unyi maneno kwa kusema kwamba 99.9% ya lawama zangu zote nazielekeza kwa ’ Mamlaka ’ husika ambayo ni TCRA.

Katika hili wala siipi lawama SERIKALI ( japo wengi wenu mnaitupia lawama ) nikiwa na maana kwamba endapo ’ Watendaji ’ wakuu wa TCRA wangetumia muda wao mwingi wa kukaa na Wamiliki wa hii Mitandao nchini Tanzania basi nadhani wangekuja na ’ something very constructive and positive ’ ambacho kingesaidia badala ya ’ kubomoa ’ kama sasa.

TCRA hata kama ni ’ chombo ’ kilicho chini ya SERIKALI bado naamini kama wangesimamia ukweli na uweledi wao ’ kiumakini ’ kabisa basi wangeweza kuishauri SERIKALI ili hii Mitandao isiwe inaonekana kama ni ’ Sumu ’ Kwao hasa ukizingatia ya kwamba hata ’ Ufanisi ’ wa SERIALI hiyo hiyo unatokana kwa kiasi kikubwa na ’ maudhui ’ ambayo yalikuwa yakiibuliwa ndani ya Mtandao wa JamiiForums.

Hakuna atakayepinga kwamba JamiiForums kupitia ’ mabandiko ’ ya ’ Anonymous Members ’ wake ( GENTAMYCINE inclusive ) kwa kiasi kikubwa mno yameweza kuwasaidia Watu wengi ( Watendaji ) huko SERIKALINI na mambo mengi sana yamepatiwa ’ ufumbuzi ’ haraka huku vitendo vingine vya Kiuhalifu na vya Kiufisadi navyo vikiibuliwa huko huko JamiiForums na tumeshuhudia yakifanyiwa Kazi na mabadiliko kuanza kuonekana.

Kuna uwezekano mkubwa sana Watendaji wa TCRA ama ni waoga au hawajui wanataka nini au wanafanya Kazi zao kwa Sifa, Kukomoa na kutafuta Maslahi fulani ndani ya Mamlaka / Tawala huku wakisahau kwamba wanachokifanya ndiyo Kwanza kinaifanya SERIKALI ichukiwe hadi kuonekana ni ya Kibabe / Kidikteta na isiyotaka kusemwa kumbe pengine hali haiko hivyo.

Nimalizie tu kwa kusema kwamba GENTAMYCINE ni ’ 50/50 ’ hivyo kama unadhani labda nipo humu ama kuisema au kuipongeza SERIKALI kwa 100% au unadhani pengine nipo humu kwa kuwasifia WAPINZANI au kuwasema nadhani pia utakuwa unakosea na niwaombeni tu acheni Kunikariri ’ na kunitupia lawama au kunipongeza kwasababu tu labda nimekidhi haja zenu za Kimtizamo / Kifikra badala yake tushirikiane kwa pamoja bila kujali tofauti zetu katika mambo ya msingi kwani Tanzania hii ni yetu sote na si ya Mzanaki au Msubi au Mchagga au Mmasai au Muha.

Wale mliokuwa mkinifuata PM nadhani sasa kwa hili ’ bandiko ’ nitakuwa nimewapeni majibu murua / sawia na tutaenda sawa kabisa.

Akhsanteni

Wenu GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE
[COLOR=rgb(184, 49, 47)]Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer

Nawasilisha. [/FONT]

Asante sana,sema chai kama kawaida

Vp? Ila umesomeka ndugu.

nimekuelewa vizuri mkuu!

Vipi kama hao tcra,wamepewa agizo kutoka juu??

Neutral means unafiki.

[FONT=courier new]Na kawaida ’ Mnafiki ’ humjua ’ Mnafiki ’ mwenzie.[/FONT]

Sawa

Hujambo?

Hauwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja

huo ni mtazamo wako

Never trust Barbarossa, Gentamycine, etc. Wako kazini.

[FONT=courier new]Yameshakuwa haya tena Mkuu? Ni Kazi gani hiyo labda Mimi naweza kuifanya wakati niko Kwetu huku Mkoani Gisenyi nchini Rwanda kwa muda mrefu sasa?[/FONT]

[COLOR=rgb(184, 49, 47)][SIZE=7]kuwa neutral ni kukosa kujua lipi positive au negative,ni dalili ya kufeli akili kuchambua, [/SIZE]

[FONT=courier new][SIZE=7]Your STUPIDITY is APPROVED![/SIZE][/FONT]

Endelea kuwa mnafiki vivyo hivyo.

nimekua mpenzi msomaji

Hili lijamaa ni linafki sana na ogopa mtu anayekwambia yuko neutral sijui hana chama ni mara elfu ya wakina @Stroke wanajitanabisha ni CCM damu.

Y

YOU ARE SMART, NEUTRAL MEANS ZERO BRAIN, MEANS SENSELESS

[FONT=courier new]Kumuelimisha ’ Mpumbavu ’ ni kujipa Kazi isiyo ya lazima![/FONT]