PAC: TSH BILIONI 27.1 MICHANGO YA WANACHAMA NSSF HATARI KUPOTEA KUTOKANA NA MIRADI 7 YA SHIRIKA HILO ISIYO NA TIJA

#1
Taarifa ya kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma (PAC), imesema kuwa shirika la hifadhi ya jamii NSSF limefanya uwekezaji usio na tija katika ununuzi wa ardhi maeneo kadhaa nchini huku taarifa hiyo ikifichua madudu yaliyofichwa na kamati hiyo kwa zaidi ya miaka 8 sasa kipindi chote ilipokuwa ikiongozwa na Zitto Kabwe (2008 - 2015)

Pamoja na madudu mengi yaliyoibuliwa na kamati hiyo ambayo huko awali yalifichwa , Bunge leo limearifiwa kuwa shirika hilo lilipata kununua jumla ya heka 28 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.85 sawa na shilingi milioni 66 kwa heka kijijini Mwandiga wilayani Kigoma jimbo la Kigoma kaskazini jimbo lililokuwa likiongozwa na mbunge Zitto Kabwe kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 ambaye miaka mitatu tu tangu kuchaguliwa kuwa mbunge alichaguliwa pia kuwa mwenyekiti wa kamati ya POAC na baadae PAC

Katika hali ya kustahajabisha ni kwa namna gani NSSF iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Ramadhani DAU iliweza kujiingiza kichwakichwa kukubali kushawishiwa kushiriki katika mradi huo usio kuwa na kichwa wala miguu mradi wa ujenzi wa ‘MWANDIGA TRANSPORT TERMINAL’ mradi uliopangwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 33.3 zinazotokana na michango wa watanzania wanaotunza fedha zao.

Katika hali ya kustaajabisha, mara zote haijawahi kutokea popote mwenyekiti wa kamati hiyo wa kipindi hicho Zitto Kabwe akikemea hata kwa kudanganya uwekezaji mbovu usiofaa wa namna hiyo kwa shirika hilo kubwa na muhimu nchini

Taarifa za uhakika zinasema bei ya sasa ya heka moja ya shamba wilayani Kigoma katika eneo la mwandiga ni kati ya shilingi laki tatu hadi milioni mbili jambo linaloshangaza zitto kuishawishi NSSF ya DAU kununua Shamba heka moja milioni 66.

Miradi mingine ambayo NSSF imeliingiza hasara shirika hilo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Apollo ya jijini Dar es salaam ambao hadi hivi sasa umeshatumia bbilioni 4.19 huku mkandarasi akiwa amekimbia site.

Mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa jingo la ubalozi na biashara vwenye thamani ya bilioni 77, mradi wa kuzalisha umeme mkuranga (mkuranga power generation) wenye thamani ya shilingin Trilion 1.15, mradi wa ujenzi wa nyumba katika eneo la kiseke na bugarika mkoani Mwanza ulioanza kutekelezwa mwaka 2008 hadi leo haujakamirika wala hautarajii kukamilika na tayari maeneo yameshavamiwa na wananchi huku zaidi ya shilingi bilioni 1.51 zikiwa zimetumika.

Mradi mwingine ulioasisiwa na NSSF ya Dkt. Dau iliyokuwa ikikaguliwa na PAC ya Swahiba wake Zitto kabwe ni mradi wa ujenzi wa nyumba katika plot namba 249 njiro mkoani Arusha mradi uliogharimu shilingi bilioni 14.7

Aidha manunuzi ya ARDHI katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam ambapo NSSF walitumia jumla ya shilingi bilioni 15.8 kununua plot 5 katika mikoa ya Dar na Pwani ambapo kiasi hicho cha fedha kilitumika kununua ardhi jiyo bila kufanyika upembuzi wa kina wa miradi iliyotakiwa kutekelezwa na shirika.

Kamati ya PAC pia imebaini kuwa jumla ya shilingi bilioni 27.1 ambazo ni mali ya wananchama zipo hatarini kupotea kwa sababu ya maamuzi ya uwekezaji usiokuwa na tija.
......
Sasa Kama Huko Mwandinga Kigoma Heka Moja Nssf Walinunua Kwa Milion 66.
.....
Je Mkoa kama Arusha si itakua Heka Milion 700.
....
Na Wakati Huo Yule Mbunge Mmoja Jimboni Yeye Ndio Alikuwa M/kiti Wa PAC na Kuna Watu Wanakuja Wanabinua Midomo Nakusema Eti Zito Ni Mzalendo.
Kiasi cha Sh27.1bilioni za michango ya wanachama katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zipo hatarini kupotea kutokana na miradi saba ya uwekezaji ya shirika hilo isiyo na tija.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Februari Mosi, 2019 bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Nagenjwa Kaboyoka wakati akisoma taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2018.

Amesema NSSF imefanya miradi ya uwekezaji ambayo umelitia hasara shirika kwa kiasi kikubwa kwani miradi mingi ilikuwa inabuniwa bila kufanya upembuzi yakinifu.

Ametaja miradi hiyo ni ujenzi wa hospitali ya Apollo jijini Dar es Salaam ambako hadi sasa zimetumika Sh4.19 bilioni lakini mradi umetelekezwa kikwazo kikitajwa ni barabara za mabasi ya mwendo kasi.

Mradi mwingine ni ujenzi jengo la ubalozi na biashara Nairobi (Kenya) ambako NSSF imeshatoa Sh854.2milioni kati ya Sh77.4 bilioni lakini hakuna shughuli yoyote inayoendelea.

"Mradi mwingine ni uzalishaji wa umeme Mkuranga ambako jumla ya Sh3bilioni zimetumika lakini hakuna kazi inayoendelea na kamati imebaini kuwa ardhi husika haijapimwa wala namna fedha za uwekezaji zitakavyorudishwa haionyeshwi," amesema Kaboyoka.

Ametaja miradi mingine ni ujenzi wa nyumba katika eneo la Kiseke na Bugarika (Mwanza) ambako hadi sasa zimetumika Sh1.51bilioni ambazo ni asilimia 80 ya Sh1.89bilioni lakini kuna tatizo katika uwekezaji wake.

Mbunge huyo wa Same Mashariki (Chadema) ametaja mradi wa Njiro jijini Arusha kuwa Sh440 milioni lakini eneo husika limevaliwa na kujengwa majengo mengi ikiwemo nyumba za ibada.

"Lakini jumla ya Sh1.85 bilioni zimetumika Katika mradi wa Mwandiga ambako NSSF ilinunua eneo la akari 28 kwa gharama ya Sh33.3 bilioni hivyo kuonyesha kila ekari ilinunuliwa kwa Sh66 milioni lakini hakuna kinachoendelea," amesema.

Mradi wa saba ni manunuzi ya ardhi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa Sh15.8 bilioni bila ya kufanya upembuzi wala kupata idhini ya bodi na ardhi husika haijapimwa.
 

sesere

Senior Villager
#3
halafu wastaafu wanaambiwa kuwa watapewa 25% ,kumbe wajanja wamezipiga hii ndo bongo,bora kuwa darasa la saba kuliko kuwa msomi tanzania
 
Top