Sasa jana nimetoka mjengo ma 5.30 jioni. Being a Friday, natembea tao kiasi. Hapo Mwembe tayari karibu Coast Bus kuna jamaa mimi huona na ma shati poa.Jamaa hua hana stall. Nikacheki ako na shati swaaafi kuruka. Nika songea karibu vile Uwesmakende husongea Momo . Akanishow nipime faster juu huwa kunakua na kanjo hutokea ghafla…Akaniuliza kama nina pesa ndogo but apparently nilikuwa na 1k. Between me and poverty. Shati tumeskizana ni rwabe. Kidogo anaulizia hawker mwenzake “change”, mmoja wao akawika “kanjo ndo haooooo”… Nilijipata nimebaki na shati nimevaa half way. Na hiyo ngiri pia imeenda…
BCE unabonga poa na jamaa wa Herzt driving school unapata stamp. Swaminarayan maisha ni ngumu. Mnalipwa per trip na ukiwa mgeni unapatiwa Tata mzee ile iwezi enda trip tatu kabla iharibike.