Rais mdogo zaidi duniani aliyeishia kunywa 'mataputapu’

Enzi zake hakushikika kwa anasa lakini sasa ni 'kula kulala’ kwa mama yake.

[ATTACH=full]180604[/ATTACH]

[ATTACH=full]180605[/ATTACH]

SIKU tatu baada ya kutimiza umri wa miaka 25 ya kuzaliwa, Valentine Strasser aliweka rekodi ya kuwa Rais mwenye umri mdogo kabisa duniani. Ilikuwa Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, aliwaongoza wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone ambako walimkuta Rais Joseph Saidu Momoh akiwa amejificha ndani ya kabati lililopo bafuni, wakamteka na kumlazimisha kuikimbia nchi yake, naye bila kubisha akachukua helikopta na kutorokea Conakry, Guinea.

Na baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda Serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).
Maisha yakabadilika. Alishakuwa mkuu wanchi. Na tofauti na matarajio ya wengine, akajikuta akizama kwenye starehe na anasa, kamwe hakuwakumbuka tena raia wake wa Sierra Leone.

Hakuangalia tena miradi ya maendeleo, lakini aliwakwaza wengi zaidi kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.

Akiwa madarakani alifuja almasi ya Sierra Leone. Rais kijana hakuambiwa kitu, ilikuwa ni yeye na starehe, starehe na yeye. Hata siku ya Wapendanao `Valentine’s Day’, yaani Februari 14 ya kila mwaka, yeye aliigeuza kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa, kwa kuwa naye anaitwa Valentine.

Pamoja na mapumziko, siku hiyo ilikuwa na chereko za kila aina, huku ikulu ikiwa na sherehe za kukata na shoka. Alikuwa na mbwembwe nyingi mno, aliyepapatikia wanawake na wakati mwingine kuua ovyo wabaya wake.

Inaelezwa hata siku ya kuzaliwa kwa Mfalme wa muziki katika miondoko ya Reggae duniani, Bob Marley (Robert Nesta Marley), pia aliifanya kuwa siku ya mapumziko kitaifa, kutokana na kumhusudu nguli huyo wa muziki aliyeaga dunia Mei 11 mwaka 1981. Bob Marley alizaliwa Februari 6, mwaka 1945.

Kwa ujumla alishaonekana kujisahau na kujiona pengine angeishika nafasi hiyo milele. Watu wake waliendelea kunung’unika, huku yeye akiponda raha ndani na nje ya bara la Afrika. Hata hivyo, ilipofika Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa madarakani na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.

[ATTACH=full]180608[/ATTACH]

Strasser akakimbilia London, Uingereza ambako aliamua kuingia darasani katika Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry ambako alianza kusomea Sheria, akisema kiu yake ni kuwa wakili ili aweze kuwatetea Waafrika.

Hata hivyo, ndoto yake iliishia njiani, kwani baada ya mwaka mmoja wa masomo, Strasser alitetereka kiuchumi, alishindwa kulipa ada na kulazimika kuacha chuo. Inaelezwa alishindwa pia kulipa pango la nyumba katika eneo alilokuwa anaishi huko Islington, Kaskazini mwa London, Uingereza.

Maisha yakawa magumu zaidi, akajikuta akilazimika kuikimbia Ulaya na kurejea Afrika mwaka 1999, akiweka makazi katika mji wa Banjul, Gambia ambako hata hivyo mambo yalimbana mno, akashindwa kulipia hata vibali vya kuishi nchini humo. Wakati fulani inadaiwa alilazimika kuishi mtaani na kuombaomba, lakini aliposhitukiwa, alitimuliwa ikielezwa pengine alikuwa anapanga kushirikiana na askari wa nchi hiyo kufanya mapinduzi.

Serikali ya Gambia iliamua kumsafirisha kurudi Uingereza mwaka 2000, lakini alikataliwa kuingia nchini humo, hivyo kulazimika kurejea Sierra Leone, hadi mjini Grafton, Mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.

Akiwa huko, kwa kuwa hakuwa na fedha wala biashara ya kuisimamia, aliamua kuanzisha chuo kidogo cha kufundishia kompyuta naTeknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). Hata hivyo, kutokana na mazingira ya chuo hicho, nacho kikamshinda. Kwa muda mrefu buibui na tandabui ndivyo vilivyoshamiri.

Na kutokana na kila kitu kwenda kombo, inaelezwa Strasser mwenye umri wa miaka 50 sasa, aliamua kurudi nyumbani kwa mama yake mzazi aitwaye Beatrice anakolelewa tena, kwa chakula na malazi.

[ATTACH=full]180609[/ATTACH]

Maisha yake kwa sasa ni pombe, yeye na pombe. Halewi pombe za gharama, bali za kienyeji ikiwa ni pamoja na pombe ya mnazi. Baa anazokunywa hazina chembe ya hadhi ya mtu aliyewahi kushika madaraka makubwa katika nchi.

[ATTACH=full]180610[/ATTACH][ATTACH=full]180611[/ATTACH]

Ni mtu wa kawaida mno kijijini kwao, anachukuliwa kama mlevi tu. Hakuna anayeshituka kumuona, zaidi ya kumkwepa pengine kwa kuhofia kuombwa fedha.

Maisha ya Strasser ni magumu mno, na inaelezwa alikimbiwa pia na mkewe Amelia. Kwa sasa Strasser hana marafiki wa uhakika, zaidi ya wamiliki wa baa. Anapuuzwa na kila mtu wakisema kwa kuwa hakuwajali wakati akiwa Rais, basi hastahili heshima yoyote kwa sasa.

Pengine huyo ndiye mkuu wa nchi wa zamani anayeishi maisha duni zaidi kuliko wote duniani. Kipato kikubwa cha Strasser katika miaka ya hivi karibuni ni fedha kiasi cha dola za Kimarekani 2,000 (Sh milioni 4.2) alicholipwa kama kiinua mgongo chake jeshini.

Alipoulizwa hivi karibuni kama ana mpango wa kurudi katika siasa, alikana akisema hana muda huo. Anatamani kurudi jeshini? “Hapana, sihitaji tena kusikia habari hizo”. Ni kauli ya Strasser akiwa katika baa ya John’s akiwa na rafiki yake na msiri wake mkubwa aitwaye Daniel.

Strasser hataki kukumbuka mengi ya nchi yake, lakini anasema hatasahau mafanikio ya timu ya soka ya taifa ya Sierra Leone katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) enzi za utawala wake. Angalau ilifika raundi ya kwanza mwaka 1994 na 1996.

Historia haipigiwi makofi…Anyway ndo maana huyu anafanya hivi asije ishi kama huyo …

Hapo kwa bob marley nampa tano

Huyu hakuwa mwizi Kwani, au ndo hizo anasa

Duh!.. :oops::oops::oops:

Anasiktisha sana…

Kila kitu kina nwisho…

Cc: @Mahondaw

“Niliwahi kuwa Rais mimi” lakini itabaki historia.

Hiyo ndio sababu hapa nchini mwetu marais na mawaziro wakuu wastaafu wanalipwa 80% ya kiongozi wa nafasi yake aliyeko madarakani. Kinyume na hapo tungekuwa na kiongozi wa hivyo pia.

Maskini Stasser alipewa akili yenye capacity ya 250kb/500gb hakuwa na namna.

nimwona hiyo picha nikamkumbuka @Tatum wa jf

aisee huyo jamaa nadhan anajuta sana maishani mwake na kama hana majuto yoyote basi atakuwa na moyo mkuu

Wanajeshi huwa hawajutiii mkuu!

good read.

kumbe Tatum anawekaga picha hii? Sema yule jamaa pamoja na ulumumba wake namkubali kitu kimoja, huwaga hapanic hata ajibiwe povu ni mtulivu, kwa ufup anabusara kias flan, nahc n lumumba wa zanzibar

Ila huyo jamaa huyo historia jinsi ilivyotata akiandikia kitabu kitamtoa kimaisha!

Aiseeehhh hili hatari kuna mtu itamrudia tena Afrika amini kwamba

:oops::oops::oops: Acha wee! Ni nani huyo?..

huyu jamaa atakuwa anajuta sana kwa sasa.

Atakuwa huyu nanihiii huyu.

Mwanajeshi anafia vitani.
Nalog off

Brare, maghaseer muko aje? Natembea hii vitongoji vyenyu