Result slip mughanga sekondari

Mwalimu mkuu na mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Mughanga sekondari iliyopo manispaa ya singida wamegoma kutoa result slip kwa wahitimu wa mwaka jana wa shule hiyo kwa madai ya kupewa kiasi cha pesa (Tsh 5000).
Naombeni ufafanuzi hii system imeanza lini?

Toa tu kwani tunakusanya kodi kwenye kila mwanya.

Mh , kama unadaiwa kalipe tu

Wahitimu wote au ni mwanao tu?

ni wahitimu wote mkuu

Tangu lini umeona result slip ikalipiwa

Hiyo hela wanayoambiwa wailipe, ni kwa sababu gani?

Ndo wamesema result slip inalipiwa haitolewi bure

Sijawahi kulipia au kusikia zinalipiwa.

Kwa shule nilizosoma na utaratibu uliozoeleka kwenye shule za serikali ni kulipia michango yote shuleni na Ada kuanzia kidato cha I hadi IV au cha V hadi VI ndio utapewa hiyo result slip na cheti, hii inazingatiwa ili kusaidia watu kulipa madeni ya Ada na michango ya shule.

Ya kulipia result slip pekee hapo hapana, labda kama kulikuwa na mchango ama wa mlinzi au taaluma ndio inaweza kuwa sawa. Jee inaweza wahitimu wote wasilipe mchango wa taaluma… jambo ambalo haliwekani.

Jaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu hilo jambo upate uhakika wa chanzo chao cha kudai hela ilipwe ndio mpewe results slip

We dogo utakuwa unadaiwa wewe, hao jamaa wa hapo nawajua

J

[QUOTE=“Kichambati-Juma, post: 1678251, member: 37851”]
Mwalimu mkuu na mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Mughanga sekondari iliyopo manispaa ya singida wamegoma kutoa result slip kwa wahitimu wa mwaka jana wa shule hiyo kwa madai ya kupewa kiasi cha pesa (Tsh 5000).
Naombeni ufafanuzi hii system imeanza lini?
[/QUOTE
Dogo huna busara… nenda kwa afisa elimu kapeleke malalamiko yako, wamekufundisha miaka minne hao halafu unajifanya mpaka matope mzuri…[/QUOTE]