RICH MAVOKO ATENGWA NA WCB, INASEMEKANA NI BAADA YA KUKATAA KUMPA DIAMOND PLATNUMZ WIMBO WA RUDI

Baada ya Superstar Richmavoko kutoonekana kwa kipindi kirefu katika camera za WCB, na kutotoa nyimbo mpya kwa mda mrefu, Tetesi za chinichini kutoka kwa watu wao wa karibu inasemekana Rich mavoko na Bosi wake Diamond Platnumz kwa sasa wamevurugana

Tetesi zaidi zinadai kwamba Mgogoro uliazia wakati Diamond akihitaji Rich Mavoko ampe nyimbo yake ya Rudi aliyomshirikisha Patoranking lakini inasemekana kuwa Rich mavoko alikataa kumpa Diamond Platnumz hiyo Nyimbo, ndipo Vuguvugu la kutoelewana likaanzia hapo

Inasemekana baada ya Mavoko kukataa kumpa Diamond nyimbo ya rudi ili aiimbe yeye, ndipo Mavoko Akaanza kutengwa kimya kimya

Dalili zilianza kujionyesha pale Crew nzima ya WCB ikiachia nyimbo mpya kila baada ya mwezi , lakini mavoko hajatoa kazi mpya kwa mda mrefu hadi mashabiki wakaanza kumshambulia kwa maneno makali kwenye Account zake za Instagram na Twitter bila kujua nini kinaendelea, hata kwenye events na show za WCB Rich mavoko hakuonekana kwa kipindi kirefu, hadi sasa Mavoko haonekani kwenye events yoyote ya WCB

L

Huyu rich acha yamkute kwenda tu wcb ilikuwa kujimaliza kabisa

Rich bana alitakiwa nae awe mtu wa majungu na kiki Mbuzi kama watu wa wcb ila sasa jamaa mpole anawaza kazi zake tu. Rayvanny anaenda nao hivyo hivyo sababu anajishusha sana ili mradi asikose pesa ya kulea mwanamke wake

Wazee Wa Kukichafua Huko Mitandao Ya Jamii Kila Siku Hawakosi Kituko Kipya
Vp Reality Show Inaanza Lini

Yani hatari rayvanny nae ugumu wa maisha tu, q boy, kifesi, mwarabu wote washapigwa chini

Imeshaanza kwa kiki ya kumtenga mtoto wa tununu kisha dai akajishtukia na kubwatuka mwenyewe kujitetea kwann mtoto hakuwepo

dia

diamond sometime anazingua

Wale wanajielewa sana. Mwarabu nadhan alikereka jinsi walivyoitumia vibaya kiki ya kusemekana anatoka na sarah wa harmo

Dstv Wapo Channel Namba Ngapi Na Marudio Ni Lini?

Sana hana msimamo. Mtoto anateseka kwa makosa yake,tununu na mama dai. Hao wana ugomvi bora wakae waombane msamaha yaishe na sio kuleta visingizio na kutukana timu walizozianzisha wao wenyewe

Kitendo cha rich kujiunga wcb ilikuwa ni kujimaliza acha apambane na hali yake

Mie mwenyewe nadakia story za insta,dstv imejaa world cup.

Ila kijana ana sauti nzuri sana…

Hivi mwarabu hajafutwa kazi kweli?

Nahisi keshafutwa au anaondolewa mdogo mdogo maana ajali aliyoipata ni kubwa sijaona boss akienda mtembelea hosp na picha juu kama kwa zama alipojifungua

Kiki kwa pikipiki,kama diamond alikuwa anataka wimbo wa mavoko si angetangaza dau tu,hivi msanii hawezi kufanya promo wimbo wake mpaka atengeneza “KIKI”?

Hapo hata mwenyewe nimeshangaa,maana bosi ni mpenda sifa lazima angempost tayari.
Maana hata eid alivyoenda kutoa zawadi tandale mwarabu sikumuona

Kingine tale na salam wameshaanza kujiweka kando kiaina au labda wameamua kupunguza mazoea binafsi na dai na kuweka mbele mazoea ya kazi baada ya kuona kijana haeleweki kama zamani