Sherehe za ushindi wa wizi wa kura Dsm! polisi na Makonda

#1
Kama kijana nayeipenda nchi yangu, nayependa amani, demokrasia na maendeleo nafanyaje?

Nafanyaje Askari wanaposherehekea ushindi wa dhulma wa chama tawala kwa kuimba 'soldier nyakua'?

Nafanyaje mheshimiwa rais anapotoa ilani ya kumshughulikia Mkurugenzi atakayemtangaza mpinzani kuwa mshindi kwenye uchaguzi?

Nafanyaje napoona viongozi wangu wa chama, wapenda demokrasia na amani, wakidhalilishwa na polisi kila leo,wakinyang'anywa Mali zao kwa nguvu, wakilazimika kuzunguka mahakamani kila uchao na wakidhalilishwa wao na familia zao?

Nafanyaje napoona vijana wenzangu wa Rika wakishawishiwa na kushawishika kwamba demokrasia haina nafasi Bali siasa za visasi, hujuma na matumizi ya nguvu ya dola ndio mtindo wa kileo?

Nitaendeleaje kuamini katika uchaguzi huru na wa haki wakati tume yenyewe ya uchaguzi haiamini Wala vyombo vya dola haviamini?

Kwanini wakati wa apartheid vijana wa Afrika kusini walikuja kujifunza hapa mbinu za uasi?
Kwanini hawakuitisha tu mikutano ya siasa nchini kwao na kwenda kupiga kura?

When democracy has no chance, it is the responsibility of everyone and anyone to give it a chance!

SOLDIER NYAKUA, NYAKUA!
 
Top