SIJAMUELEWA MELLO HAPA WANDUGU KWA MANENO HAYA YENYE KULENGA KITU AU MTU

Maxence M. Melo‏Verified account @macdemelo 3h3 hours ago
More
In almost every profession - whether it’s journalism, finance, medicine or running a small business - people rely on confidential communications to do their jobs. We count on the space of trust that confidentiality provides. When someone breaches it, we are all worse off for it! NICE tweeting

miongoni mwa kanuni za “maudhui” ni kuweka wazi chanzo cha taarifa yoyote unayeipakia mtandaoni. hivyo kunakua na breach of confidentiality, so nadhani mello anasisitiza madhara ya hizo kanuni kwenye tasnia ya habari mitandaoni

Ooh! Sawa

Kuweka wazi chanzo cha taarifa unayoipakia

Hapo mbona jela inakuita wazi wazi.

Kwa mfano umeweka taarifa "Jiwe limesema tufyatue tu "chanzo Wewe mwenyewe ulikuwa kwenye mkutano, Baadaye Ikulu inakuja kukanusha na Rais hakusema hivyo alinukuliwa vibaya.

Hapo tayali unacho.

Hizo ni code of conduct kwa taaluma yoyote…kuna watu anajaribu kuwaamsha usingizini japo wataona ni ukweli wanaambiwa Ila watang’ang’ania tu kuwa wako sahihi…hebu fikiri pale home kwako ikitokea umefanya ndivyo sivyo huwa unakubali moja kwa moja?

Siendi JF(Tz). Bora niendelee kubakia hukuhuku Kenya. WAcha wabaki wenyewe. Wakirudi nitakuwa na access ya read only

Haha naona unakwepa kwenda jela.

Kipi hujaelewa mkuu?

Hii inamaanisha Hata ukiisajili haitakua na maana kwa upande wa security ya watumiaji

Unakuta watu wanaotaka kupata taarifa za siri za watu humu ndani, ndio hao wanaficha mikataba ya raslimali za nchi ambazo ni za wananchi wote!! Mello usikubali hizo sheria za wahuni wenye uchu wa madaraka. Acha tubaki hukuhuku uhamishoni tufanye yetu.

Tanzania

Source maana yake si ku disclose jina halisi la mtu; mtu kasema hiki na vymbo vya habari vikachuja bila kurusha lakini waliokuwepo wakairusha mtandaoni na ukaona kabisa aliyeoongea. Hapo utahitaji source ya kazi gani au aliyerusha unamtafutia kitu gani?

wanaolengwa na hiyo kanuni ni whistleblowers, fuatilia kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya JF, miongoni mwa mashtaka ni mwendesha mashtaka anataka taarifa za mtu (mwana JF)aliyetoa habari ya ukwepaji kodi wa oilcom bandarini. kwa sheria za zamani ile kesi haiendi kokote, na ndio maana zimetungwa hizo kanuni. kwahiyo ikitokea unataka kufichua taarifa flani ya siri lazima utajulikana kuwa ni wewe uliyeitoa.

Kwa jinsi mimi nimemwelewa jamaa ana claim uhuru na usiri wa taarifa kwenye mawasiliano ambacho ndio tatizo kuu hii mitandao hivi sasa inatakiwa kutoa taarifa za watumiaji wake kwa serikali wakati wao (Mello) hawapo tayari kwa hilo kwasababu sio sahihi kubanwa kwa haki ya kujieleza kupitia vyombo vya habari.

Atakae elewa hiyo lugha ya bepari, naomba anifanyie tafasiri tafadhali

Ana maana ya kwamba… hakubaliana na swala la members wake kuweka taarifa zao hadharani…

Cc: @Mahondaw

KATIKA KAZI YOYOTE KIMAADILI KUTOA TAARIFA ZA MTEJA WAKO HAIFAI NI SIRI BAINA YENU