Sijuti wa KenyaTalk aandikwa na Mwananchi online

Dar es Salaam. Siku chache baada ya mtandao wa Jamii Forums kusitisha huduma zake, umebainika unafanya kazi kwenye mtandao maarufu wa Kenya Talk wa nchini Kenya.
Juni 11, Jamii Forums ilisitisha huduma zake kutokana na tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Juni 10, TCRA ilitoa notisi ikielekeza kuwa ni kosa kisheria kutoa na kuchapisha taarifa kwa njia ya mtandao bila kuwa na leseni ikitoa hadi Juni 15 kutekelezwa kwa sharti hilo.
Hata hivyo, akizungumza kwa simu na Mwananchi, mkurugenzi na mwanzilishi wa mtandao huo, Maxence Melo alikanusha kuihamishia Jamii Forums nchini Kenya, akisema hawana makubaliano na waliouhamisha.
“Hatujahamishia Jamii Forums Kenya, hao wanaoendesha jukwaa hilo inawezekana wameona Tanzania imezuia sauti za watu kwa hiyo wamezichukua wao. Kama sauti zetu zinazuiwa, wengine wanachukua wanaendelea,” alisema Melo.
Huku akitoa mfano wa wafanyabiashara, Melo alisema nchi za jirani zinatumia matatizo yanayotokea Tanzania kujinufaisha.
“Kwa mfano kuna wakati wafanyabiashara walikuwa wanalalamikia mazingira mabovu ya biashara, hawakusikilizwa, wakaamua kwenda Kenya kuwekeza hisa zao,” alisema Melo.
Alisema tangu walipoamua kusitisha huduma zao , wamefanya jitihada za kuzungumza na TCRA bila mafanikio hata hivyo alisema wataendelea kuwatafuta ili kupata suluhisho.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Jamii Forums inapatikana katika mtandao wa Kenya Talk. Katika ukurasa wa Kenya Talk wa yaliyomo kuna orodha ya majukwaa mbalimbali ikiwemo Jamii Forums.
Ndani ya Jamii kuna majukwaa yaleyale yaliyokuwemo ikiwamo Jukwaa la Siasa, Jamii Intelligence, habari mchanganyiko, biashara, uchumi na ujasiriamali, mahusiano, mapenzi na urafiki, international forum, utani, michezo na burudani.
Katika jukwaa la siasa, miongoni mwa mada zilizotumwa ni pamoja na ‘hivi malaika waliosemwa hapa ni akina nani?’ ambayo wachangiaji mbalimbali wanaojitambulisha kuwa Watanzania wameendelea kuchangia.
Mchangiaji mmoja anayejitambulisha kama ‘Sijuti’ ameweka nukuu ya Rais John Magufuli aliposema : “Nilikuwa natamani siku moja malaika washuke waizime hii mitandao yote, ili baada ya mwaka mzima itakapokuja kufunguka wakute sisi tumeshatengeneza Tanzania yetu mpya.”

Hivi karibuni viongozi wa Jamii Forums walioshitakiwa akiwemo Melo wameshinda kesi moja kati ya tatu zilizofunguliwa na Serikali.
“Tumeshinda kesi moja kati ya tatu zilizokuwepo. Nadhani baada ya kuona wameelemewa mahakamani ndiyo wameamua kutufungia. Inawezekanaje mamlaka inayokusimamia ndiyo hiyo hiyo inayotunga kanuni za kukushitaki?” alihoji Melo.

Uzi waliozungumzia ni huu>>>Hivi malaika waliosemwa hapa ni akina nani?

Chanzo: [B]Mwananchi[/B]

Majukwaa yanarudi taratibu… mpaka yote yatahamia huku…

Sasa nao, tunafuatana fuatana mpaka huku…

Cc: @Mahondaw

Yap

Karibuni sana, lakini msiwaache madem wenu nyuma. Kujeni nao pia

Nami natoa shukran zangu za dhat kwa Mwananchi. Maana singeijua Kenya talk Kama sio waiting. Hongera kuwah @Sijuti

Kabisa

Aiseee

Tuanaomba tu wasije kuingia hadi huku maana watatafuta namna ya kuweza kudhibiti KT Tanzania

Asante kwa taarifa

Mavileja mupo!!hahahaaaa

Malaika mzima mitandao asifike huku

joseverest umefikafikaje huku?

Aah kitambo sana Mwaka Jana 2017 nilijiunga huku

Naona tayari mwenzetu umeshakuwa mzee wa kijiji!!

Karibu kiongozi naona ushakula cheo cha “laibon” hahaha ughaibuni raha

Watafika tu siku si nyingi

Haaaahaaaaa. Malaika mzima mitambo. Pumbavuuuuuuuu zaooooo.

melo aje achonge nao jamaaa mambo yetu jf original aunganishe huku.

Jamaa ovyo sana wale
Nalog off

Sawa mzee wa Mwananchi pia kuna Mwifwa mzee wa BBC