Simba S. C. Yawasajili Meddie Kagere, Serges Pascal Wawa na Deogratius Munishi (Dida)

Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salam imefanikiwa kumsajili mshambuliaji raia wa Rwanda, Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya nchini Kenya.

Mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake na Gor Mahia unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu, amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru na anatarajia kuonekana akiwa na jezi ya Simba kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki inayotarajia kuanza kutimua vumbi hapa nchini June 28.

Aidha, imeelezwa kuwa Kagere amesaini kwa dau la dola 50,000 sawa na zaidi ya shilingi million 110 za kitanzania huku mshahara wake ukitajwa kuwa ni dola 5,500 ambazo sawa na zaidi ya shilingi milioni 12 zakitanazania.

Wengine waliotambulishwa ni pamoja na Serge Wawa na Deogratius Munishi waliosajiliwa hivi karibuni, pia Adam Salamba, Mohamedi Rashid na Marcel Kaheza ambao walisajiliwa mapema wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa.

[ATTACH=full]180318[/ATTACH]

Usajili wa kimihemko

Kwa sasa kwenye Nafasi ya ushambuliaji Simba itakua na John Bocco, Emmanuel Okwi, Adam Salamba, Mohamedi Rashid na Marcel Kaheza, Meddie Kagere

Ndo mana nikasema usajili wa kimihemko, manara kachukua nafasi ya Hanspope

ni kocha kawataka au ni viongoz wamesajil tu! naona mapichapicha tu

Wapewe na Mikongojo, vibabu fc

Manara ndo kawataka, kocha si alishatimuliwa

inasikitisha sana… afu watakaa bench msim mzm kam akina niyonzima