Simulizi:Viganja mikononi mwangu

nyemochilongani SEHEMU YA 01

Cassian alikuwa kimya, macho yake yalikuwa yakiangalia baharini huku mawazo yake yakiwa mbali kabisa. Moyo wake ulichoka, maumivu aliyokuwa akiyasikia moyoni mwake hayakuweza kuelezeka.

Alikuwa bilionea mkubwa, mwenye makampuni mengi, migodi ya dhahabu na kila kitu ambacho kingemfanya kustahili kuitwa bilionea. Alimshukuru Mungu kwa utajiri aliokuwa nao lakini tatizo lilikuwa moja tu, hakuwa na mtoto.

Hilo lilikuwa pigo kubwa katika maisha yake, wakati mwingine alikuwa akimuuliza Mungu juu ya kilichokuwa kimetokea. Kwa nini alimpa utajiri mkubwa na kumnyima mtoto? Utajiri ungekuwa na maana gani kama tu hakuwa na mtoto ambaye angekuja kuurithi baada ya yeye kufa?

Hakuwa na furaha hata kidogo, kila siku moyo wake ulichoma kama moto kiasi kwamba alimuonea aibu mkewe, hata kukutana naye wakati mwingine aliogopa kutokana na tatizo lililokuwa mwilini mwake.

Hapo ufukweni mawazo yake yalikuwa mbali kabisa. Alitulia ndani ya gari huku akionekana kuwa na mawazo lukuki, alikaa garini kwa dakika kadhaa ndipo akaamua kutoka na kuanza kutembea.

Kwa jinsi alivyokuwa akiwaza mpaka wakati mwingine machozi yalikuwa yakimtiririka mashavuni mwake.
Aligombana na dada zake kwa sababu hakuwa na mtoto.

Kipindi cha kwanza ndugu hao walifikiri kwamba mwanamke aliyekuwa akiishi naye ndiye alikuwa na matatizo lakini baada ya kupima katika hospitali tatu, zote zilionyesha yeye ndiye alikuwa na matatizo.

Hakutaka kuwaambia ndugu zake ukweli, alikuwa tayari kugombana nao na hata kuchukiana maisha yake yote lakini si kuwaambia ukweli kwamba tatizo la kutokupata mtoto lilisababishwa na yeye na si mpenzi wake kama walivyokuwa wakihisi.

“Kwa nini wanamuonea? Kwa nini hawataki kuniuliza ili wajue ukweli kwamba Evelyne hana tatizo?” alijiuliza huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Moyo wake ulimuuma mno, hakuona thamani ya utajiri, bila kuwa na mtoto maisha yake yangekuwa hivyohivyo mpaka kifo chake na mali kubaki kwa ndugu zake.

@carbamazepine @Madame S @moneytalk @Tumosa @Jackal2 @Jackal1

SEHEMU YA 02

Si kazini, si nyumbani au barabarani, kila alipokuwa Cassian alikuwa myonge, hakuwa muongeaji, wakati mwingine alihisi kabisa mwili wake ukianza kupungua kutokana na matatizo aliyokuwa nayo.

Alipenda kuwa na mtoto, kila alipowaona wanaume wenzake wakiwa na watoto barabarani moyo wake ulimuuma, alitamani kuona kama ingekuwa yeye, alitamani kuona naye akiwabeba watoto wake kama walivyofanya watu wengine.

Mpenzi wake ambaye alimchukulia kama mkewe, Evelyne ndiye aliyekuwa akimfariji kila siku, alimwambia kwamba hakutakiwa kukata tamaa na ipo siku ambayo Mungu angetenda muujiza na hatimaye kupata watoto.

Alimwangalia Evelyne machoni, aliyaona maumivu yake, aliona jinsi msichana huyo alivyokuwa akiumia kwa kuwa tu hakuwa na mtoto. Alimuona kuwa mwanamke mwenye uvumilivu sana, aliyevumilia maneno ya ndugu na wakati hakuwa na tatizo bali tatizo kubwa lilikuwa kwake.

“Pole sana mke wangu,” alisema Cassian huku akimwangalia Evelyne.
“Usijali mume wangu! Maneno ya watu huwa hayanisumbui hata kidogo! Mimi nimekupenda wewe, katika shida na raha hakika tutaendelea kuwa pamoja na kamwe sitokuacha,” alisema Evelyne maneno ambayo kwa Cassian yalionekana kuwa faraja kubwa.

“Ila sina uwezo wa kumpa mimba mwanamke!” alisema Cassian.
“Hata kama! Nimekupenda wewe mpenzi, mtoto ni majaaliwa ya Mungu,” alisema Evelyne huku akimwangalia mpenzi wake huyo machoni mwake.

Japokuwa mkewe alijitahidi sana kumfariji lakini hakufarijika, bado alijiona kuwa na mzigo mkubwa kichwani mwake. Alimuomba Mungu kila siku bila kukoma, maombi yake makubwa yalikuwa ni kupata mtoto.

Ni kama alimuona Mungu akiwa ameziba masikio, alijitahidi kufunga na kuomba lakini matokeo yalikuwa yaleyale kwamba hakupata mtoto.

Hilo lilimuuma mno, alichokifanya ni kwenda kwa madaktari wengi pamoja na mkewe, katika kila hospitali aliyofika, aliambiwa kwamba alikuwa na tatizo kubwa katika mfumo wa utengenezaji mbegu, hazikuwa na nguvu za kumpa mimba mwanamke.

SEHEMU YA 03

Kila aliposikia sehemu kuna mikutano ya injili, yeye alikuwa wa kwanza, wakati mwingine alimuacha Evelyne nyumbani na kwenda huko, alitaka kumuona Mungu akimtendea muujiza lakini alimuona Mungu kuchelewa kwani kwenye kila alipofanyiwa maombezi aliambiwa kabisa kwamba angepata mtoto lakini matokeo yalikuwa yaleyale, hakupata mtoto.

Maumivu hayakupungua moyoni mwake, alikuwa mtu wa majonzi na kulia kila siku. Hakuona thamani ya utajiri, wakati mwingine alimwambia Mungu kwamba alikuwa tayari kupoteza kila kitu lakini mwisho wa siku aje kuwa na mtoto lakini maombi yake yote hayo yalionekana kama si kitu mbele za Mungu.

“Mchungaji! Kwa nini Mungu hajibu maombi yangu?’ aliuliza Cassian huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Kuna siku atafanya jambo. Nakwambia kwamba kuna siku utapata uzao wako wa kwanza,” alisema mchungaji huku akimwangalia Cassian.
“Kweli?”

“Unachotakiwa ni kuamini. Uwe na imani hata kama ni ndogo kama mchanga, hakika Mungu atafanya jambo,” alisema mchungaji huku akimwangalia Cassian.

Aliteseka usiku, hakulala vizuri, kila wakati alikuwa akishtuka usiku na alipoyafumbua macho yake kitu cha kwanza kilikuwa ni mtoto tu. Evelyne alimuonea huruma, wakati mwingine msichana huyo aliinuka kutoka kitandani na kwenda sebuleni, huko alikuwa akilia kama mtoto, hakuamini kama alikuwa akipitia maisha yake, alimpenda sana Cassian, alitamani siku moja wawe na familia yao lakini jambo hilo lilishindikana kabisa.

Cassian alipokuwa akiamka na kumkosa mkewe kitandani, alimfuata sebuleni na kumkumbatia, alimfariji kwa kumwambia kwamba kuna siku wangepata watoto hivyo hakutakiwa kuwa na hofu hata kidogo.

“Kuna siku Mungu atatupa familia yetu! Usilie mpenzi, amini kwamba kuna siku tutakuwa na familia yetu,” alisema Cassian huku akiwa amemkumbatia Evelyne.

“Ninaamini mume wangu!” alisema Evelyne huku akilia kilio cha kwikwi.

@Sakayo @Mahondaw @Smart911 mkuje mambo yameanza

Abeeeeee

Tulia usome story sasa

Asante sana kwa hekaya

Santo sana mamiii ngoja nisome

cc @Smart911

Sawa babe

Usisahau kumwita mbebez wako

Endeleaaa mekuja nzur

Usijali Atakuja sema leo alikuwa bize kidogo

Cc @Smart911

Tutaendelea mama usiwe na presha

Okay maa

Duniani kila mmoja na shida zake jamani ukiona umepewa vyote mshukuru sana mungu kwa neema hio…

ngoja nimalizie kwanza

cc @Smart911

Mungu ni mwema… naamini atapata mtoto tu… ngoja tuone shunie ataamuaje ‘’

naendelea kusoma…

cc @Smart911

Acha tu kila mtu ana mitihani yake

Shunie Nimependa uvofupisha fupisha hizo scenes make ndefu zinashoshaga kusoma teh…

cc @Smart911

Woooooooozeeeerrrrrrr nipo hapa maa,nafuatilia kama kawaida