SIRI YA MNANGAGWA KUTEMBELEA TANZANIA.

Habari zenu…
Hizi ni sababu Kuu mbili zilizomleta MNANGAGWA, Emmerson Humu nchini.
1.Kuomba ulinzi kwa serikali ya Tanzania
2.Kuomba maafisa ambao watamfundishia maafisa wake namna y ufungaji bora wa goli la mkono.

NINI TUTEGEMEE?
1.ULINZI wa MNANGAGWA kuimarika zaidi.
2.Siasa chafu /za maji taka
3.kuuwawa, kuteswa na kupotezwa kwa wanaompinga yeye na serikali anayoongoza.
4.Ushindi katika uchaguzi ujao kwa asilimia zaidi au karibu na 63.7
5.maofisa wa vyama tawala kuitembelea nchi moja wapo.
6.mkuu wa majeshi nchini Kuwa mgeni au mwenyeji wa mwenzake.

Baada ya uchaguzi mkuu wa zimbabwe.
1.kutakuwa na vipindi vifupi au virefu vya vurugu.
2.Serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa.

WAIT and SEE YOURSELF.

hapo ushindi ni zaid ya 80%,ngoja tuone wataongea nin.

Hapo yajayo yanasikitisha

anakuja kupewa mbinu chafu na jiwe jinsi ya kudili na wapinzani wake. lazima awapoteze. viroba style.

Huu ni utabiri

Kaja kuchukua notes za kufunga bao la mkono

Nape ataalikwa au?

Amekuja matembezi tu, Utalii

Atakwenda kutoa semina kama mjumbe mjowapo wa kutoka halmashauri Kuu ya CCM.

Hakuna cha siri wala nini, anachofanya ni ziara tu kama ziara nyingine za viongozi… maana kabla ya kuja nchini amekwisha tembelea nchi za Namibia; Zambia; Msumbiji; Angola, Afrika Kusini; DR Congo na Botswana. Je, huko nako alikuwa na siri gani? Wabongo tunapenda kukuza mambo…

Anakuja kukutana na jiwe gumu

Kwamba anakuja kupewa ushauri na jiwe

Ila kwa Mbio za wale Walinzi inabidi tuwape mafunzo maana ni hatari kuwa na type za walinzi design ya kina Harmorapa.

ingekua wewe pale ungefanya nini

Huenda kwa kuwa anakuja muda mfupi kabla ya uchaguzi wa nchi yake, na mwenyeji wake ambaye ni rais wetu hana rekodi nzuri kwenye uchaguzi huru na wa haki. Na kwa mazingira yalivyo hakuna namna katika mazungumzo yao hawataongelea uchaguzi wa hivi karibuni wa Zimbambwe hata kama sio lengo la hiyo ziara.

Kwa ujumla timing ya hiyo ziara haijakaa pazuri, kiasi kwamba ni rahisi watu kuguess kwamba rais wa Zimbabwe anaweza kupewa mbinu ovu ambazo pia hutumika na chama cha rais wetu ambaye ni mwenyeji wake.

Tunaendelea kusubiri ili tujionee!
Nalog off

Mno!

Inawezekana, hasa kwenye hilo la mbinu za uchanguzi na kudhibiti wapinzani…

Mbinu walizokuwa nazo CCM kushinda chaguzi ni za ku-brute force; kwa afrika zinafanya. Wastaarabu na wanaojitambua wanatumia intellectual strategies. Hopeless leaders wanaweza kuja kujifunza ujinga.

Mkuu unategemea mtu aliyefanya kazi kwa muda mrefu na Mugabe na akafiti kwenye tabia zake atatumia mbinu za maana? Huyo Munangagwa mbinu za ushindi za ccm zinamlipa sana kwani sio mtu anayeweza kushawishi wananchi hasa ukifuatilia mwenendo wa serekali aliyokuwa anaitumikia.