Swalah ya Janeza

[SIZE=6]Kumtayarisha Maiti[/SIZE]
Inapendekezwa kuhudhuria pale penye mtu ambaye alama za kifo zimedhihiri kwake, na kumkumbusha kusema «Laa ilaaha illa-llah» kwa kauli yake Mtume ﷺ (Walakinini maiti zenu “Laa ilaaha illa- llaah”) [Imepokewa na Muslim.].

Akifa atafumbwa macho yake na afinikwe nguo na kufanywe haraka kumtayarisha kwa mazishi na kumswalia na kumzika.

[SIZE=5]Hukumu ya kumuosha maiti na kumtayarisha na kumzika[/SIZE]
Kumuosha maiti, kumkafini, kumbeba, kumswalia, na kumzika ni katika faradhi inayotosheleza. Wakifanya baadhi ya waislamu inapomoka madhambi kwa waliobakia.

[SIZE=5]Hukumu ya kumuosha maiti[/SIZE]

  1. Yatakikana achaguliwe mtu mwaminifu wa kuosha maiti, pai awe mjuzi wa hukumu za kuosha.

  2. Hutangulizwa kuosha yule mtu ambaye maiti mwenyewe alikuwa ameusia aoshwe na yeye. Kisha yule aliye karibu zaidi na maiti, iwapo ana ujuzi wa hukumu za kuosha. Akitokuwa hivyo, basi atatangulizwa mwenye ujuzi wa hilo.

  3. Mwanamume huoshwa na wanaume, na mwanamke huoshwa na wanawake. Na kila mmoja miongoni mume na mke anafaa kumuosha mwenzake, kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia›Aishah t: (Hakuna cha kukudhuru, lau wafa kabla yangu nikakuosha, nikakukafini na nikakuswalia kisha nikakuzika) [Imepokewa na Ibn Maajah.].

Pia inafaa kwa wanaume na wanawake kuwaosha watoto walio chini miaka saba. Na haifai kwa Muislamu - awe mwanamume au mwanamke- kumuosha kafiri, walakubeba jeneza yake wala kumkafini wala kumswalia, hata kama ni jama yake wa karibu kama vile baba.

  1. Shahidi aliyekufa vitani haoshwi wala hakafiniwi wala haswaliwi, bali huzikwa na nguo zake.

  2. Afikapo tisha- naye ni mwana aliyetoka kwenye tumbo la mamake kabla ya kutimia umbo lake, awe ni mwanamume au ni mwanamke- miezi minne, ataoshwa, akafiniwe na aswaliwe. Kwani yeye baada ya miezi minne huwa ashakuwa na umbo la binadamu kamili.

  3. Maji ya kuoshea maiti ni sharti yawe ni maji yanayofaa kujitwahirishia na yawe ni ya halali, na aoshwe mahali pa sitara, na haifai kuhudhuria asiyekuwa na mafungamano yoyote na kumuosha maiti.