Taarifa-tutakutana na Melo muda si mrefu,soma.

TUTAKUTANA MELO.

1)Namanga hadi Holili,tunarejea nyumbani
Twarudi na zetu hali,na furaha vifuani
Safari yetu ya ghali,ila bado na imani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

2)Tutapeana mikono,na kukumbuka zamani
Tulisaga visigino,kwenye kambi ya amani
Asopenda malumbano,aliitia kizani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

3)Japo masaa machache,tutakuwa safarini
Tusubirini pakuche,tukaingie garini
Ugenini tupaache,maana hatupaamini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

4)Tutaimba na kucheza,nyimbo zetu za nyumbani
Japo sana tutawaza,wale watu wa medani
Jinsi watavyo chunguza,ili watutie ndani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

5)Tusihofu tutarudi,japo hatujui lini
Tushukuru tuna budi,na tuweke akilini
Tufanye sana juhudi,turejee salimini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

6)Tutausema ukweli,kila kona duniani
Usikike hadi mbali,Arabuni na barani
Amerika na tusali,tumrudie Manani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

7)Tutampa na salamu,za kule ukimbizini
Hali ilikuwa ngumu,ila tungefanya nini
Siku tukitia timu,tutaeleza kwanini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.

SHAIRI -TUTAKUTANA NA MELO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
[email protected]

Dereva akae nyuma
Abiria tuwe mbele
Tupige vigelegele
Tukishafika salama…

Shairi zuri

Majizi yataumia, kwa ushindi asilani
Polepole atanuna, Lumumba watakaa
Jiwe litasikia, nakutambua yupo MUNGU
Tutainua bendera, na Melo kuonana.

Good! nondo za kuingia studio kbs!

Asante sana yaani sio kwa kunifurahisha hivyo

Kumbe ni shairi/utenzi!!!

KUMBE[SIZE=1] ulijua ni ugali [/SIZE]

kwa Mara ya kwanza nagundua kuwa na wewe NI mtunzi.
hongera kwa kuwepo kona zote.

Exile is not death.
Tutarudi nyumbani
ushindi nyusoni.

Haaa haaa Mkuu umeshafika huku.

Wa mbele muiname wa nyuma tupate kuona
Nalog off

Sawa

Mbele hapako salama
Ka’ nyuma utachutama
jiwe njiana kuzama
turudie zetu zama

Aisee chama wasalimie hapo tengeru

karibu ukimbizn mtani
urewed

acha ma2c

Mkuu, ujue Mungu yuko na sisi?

Melo Yuko jukwaani halafu watu wa mbele wamesimama sasa sisi wa nyuma hatuoni,kwahiyo lzm wao wainame ili nasi tupate kumwona Melo akitupa neno kuhusu JF hiyo ndio maana yangu Mimi
Nalog off

Zimefika.