Tanzania SGR updates

Ujenzi unaendelea kwa kasi ya kutisha [ATTACH=full]178752[/ATTACH][ATTACH=full]178751[/ATTACH][ATTACH=full]178750[/ATTACH][ATTACH=full]178749[/ATTACH][ATTACH=full]178748[/ATTACH][ATTACH=full]178747[/ATTACH]

Maelezo tunaona picha au mitambo ni wapi makutupora,soga, llala funguka

Pongezi sana kwa wakandarasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ingawa Heche anadai hakuna hata senti moja ya serikali iliyotumika.

Huo ni mkopo Mkuu ambao tutawajibika kuulipa kabla SGR haijakamilika

Taifa haliendelei bila kukopa.
Huwezi kuwa mfanyabiashara mkubwa bila kukopa. Hata mzee R. Mengi alishasema hilo na kushauri vijana wasiogope kukopa na kwenda kuwekeza.

Hivyo kwa mradi huu serikali inawekeza.

Marekani pia inakopa na ina madeni kibao.

Mleta uzi anasema ujenzi unaendelea kwa kasi ya kutisha lakini haonyeshi wala kueleza imefika umbali gani tukajionee wenyewe. Ataje asilimia ngapi mpaka sasa na aseme imefika wapi. Sasa hv hatuandikii mate. Serekali hii ni waongo na hilo liko wazi, hivyo kila kitu lazima tuone wenyewe. Hadanganywi mtu safari hii.

mbona SGR haionekani kwenye picha :D? naona mtambo wa kokoto na barabara ya lami! au tumepigwa tena?

Kukopa si jambo la ajabu,tatizo serekali hii imekopa sana kiasi cha kutishia uhuru wetu.

Haijakopa kuliko serikali ya Kenya mkuu.

Bado deni la serikali ya TZ lipo ktk kiwango kinacholipika na kuruhusu kukopa zaidi.

Uko sahihi, ila hoja ni % ngapi mpaka sasa? Tuna uwezo wa kwenda kujionea wenyewe. Mwezi wa tatu nilijionea mradi ulipofika kipande cha Dar-Moro. Bado hauridhishi kulingana na mbwembwe za majukwaani zilivyo.

Uko sahihi, ila hoja ni % ngapi mpaka sasa? Tuna uwezo wa kwenda kujionea wenyewe. Mwezi wa tatu nilijionea mradi ulipofika kipande cha Dar-Moro. Bado hauridhishi kulingana na mbwembwe za majukwaani zilivyo.

Tatizo ni kukopa nabkuwekeza ktk miradi kama ya mwendokasi na kuitelekeza bila kuisimamia ifanye vema irejeshe pesa iliyokopwa na kuleta tija kwa taifa(jamii) husika.

Inawezekana upo sahihi kuhusu hatua ya mradi ulipofikia kuwa sio ya kuridhisha. Lakini mimi sijui mkataba unasema vipi kuhusu muda wa kukamilika kazi na maendeleo ya mradi kila hatua.

hairidhishi embu jipange uje upya usijekuta tumepigwa tena! bcoz hapo naona barabar tu.

[COLOR=rgb(184, 49, 47)]Kenya hata kama wamekopa kuliko sisi wao uchumi wao ni bora kuliko wetu. Hizo hadithi za kwamba tunakopesheka tumezisikia sana. Je kinachokopwa kinaendana na matokeo? kuna ajira mpya? maisha ya wananchi yameboreka?

Mkuu nashukuru kwa uchangiaji wako wenye wingi wa busara. Ni hivi mkataba hauko wazi hivyo huko achana napo. Lakini lengo la serekali ni hadi kufika 2019 kipande cha Dar-Moro kiwe kimeisha, debe la kura lifanyanye kazi. Lakini uhalisia hauakisi hilo. Ila maelezo ya jukwaani ni kama huo mradi umebakiza wiki kuanza.

Ukiangalia sababu ya kuweka jiwe la msingi kipande cha Moro-Dom ilikuwa ni political gain kwani ukweli hela hakuna na lengo ilikuwa ni kuchota wananchi mawazo kwamba kuna jambo serious linafanyika.

Uhuni wa hivyo ulifanyika wa kutangaza tender ya mradi wa SG ili kuwakoga watu, ukweli ni kuwa hakukuwa na hata senti tano ya huo mradi. Tulisema utangazaji ule wa tender ulikuwa ni hadaa ya wazi kwani rais alikuwa anajigamba kwamba pesa ya huo mradi zipo cash. Lakini ajabu baada ya muda tukasikia serekali inakopa bank ya dunia na bank ya Africa kwa ajili ya huo mradi!! Ogopa serekali liyookota vichwa vya treni bandarini kwa kukosekana mmiliki kisha ikaenda kuvinunua tena bila kutangaza tender wala kumtaja mmiliki wa hivyo vichwa. Simply nothing serious in this government. Tumehoji sana humu mitandaoni huo utapeli wa wazi kwani vyombo rasmi vya habari havithubutu kama ilivyokuwa kabla ya hii awamu. Matokeo yake ndio leo tunahoji kupitia nje ya nchi.

Ndio ipi katika hizo picha:oops::oops:

Mkuu kwenye post namba 15 naona nimekupa kitu kinauma umeishia kutoa like. Nilitaraji ungeendelea na mjadala nikuongezee madini ili ujie kwanini mitandao imewekewa sheria yenye nia ovu. Huku ni eneo la hard talk ndio maana huwezi kuona kiongozi yoyote anathubutu kuingia humu kijibu hoja.

Sana utamuona rais kajigeuza kasisi/shehe anahutubia na kusubiri kushangiliwa tu lakini hakuna kuhoji. Huko bungeni ndio vichekesho vya karne. Waziri anaulizwa swali la msingi, linalohitaji majibu ya kona, bila aibu spika anamwambia waziri ajibu kwa kifupi sana kwa sababu ya mda. Waziri anajibu mambo ya ajabu hata kama hayaridhishi lakini imetoka hiyo. Kwa sababu hiyo ya serekali kutokujibu kwa usahihi huko bungeni ndio unaona mafuta yamepanda bei, samaki kumla ni bora ukutwe na madawa ya kulevya. Sukari imeoanda bei na hela za korosho ndio utata mtupu. Bunge limegeuka kibogoyo haliwezi kuikanya serekali kwenye uhuni wake.

Ukitaka kujua mtanzania ni kichekesho kwenye hii dunia unakuta bei ya mafuta ya kula, sukari, samaki imepanda kwa approach za serekali lakini rais anasimama hadharani anasema anapigania wanyonge na watu wanalipuka kwa shangwe. Halafu rais kwa mzuka anatoa milioni kadhaa kumfariji mama mjane aliyeporwa kiwanja!

Maajabu hapo hayajaisha. Jana rais wa nchi anasimama hadharani anapokea gawio la 1.5b toka shirika la umma lenye 40yrs+, anasema hizo hela zinaenda hazina zitalipa ada bure, zitajenga reli, zitatoa huduma ya afya. Wakati huohuo serekali yake haina maelezo ya 1.5t kupitia mkaguzi wa hesabu za serekali. Halafu mtu anatokea anakuambia nchi hii imepata rais iliyokuwa inamuhitaji. Hapo Tanzania itaacha kuingia kwenye Guinness book?

Salute sana Mkuu @Tindo

Mkuu hakuna ambae anakataa Serikali kukopa hata kidogo…
La muhimu iwe ni mikopo yenye riba nafuu.

Sasa currently tumesikia Serikali imekuwa inakopa kwenye Mabenki ya Biashara ambayo kwanza riba yake ni kubwa na secondly muda wa kaunza kuu-service mkopo ni mfupi sana hivyo kwamba, lets say kama tumekopa kwa ajili ya SGR tutaanza kuuservice mkopo kabla hata Ujenziwa SGR haujakamilika with higher interest rates.

Kwanini serikali haichukui Concessional Loans ambazo terms zake are substantially more generous and affordable than Business Loans??
Au hawa watu akina Dr Mpango na wenzie wanapata vi percent wanapoenda kwenye hii mikopo inayotolewa na Mabenki ya Biashara?

Hicho ndio watu tunachopiga kelele.

Hii mikopo ni burden kubwa sana kwa walipa kodi wa Tanzania huko mbeleni.

Reli ipo wapi hapo?

Where and how can I prove kwenye hizo picha zako kwamba huu ni ujenzi wa SGR?

Maana hata kwenye migodi pia kunakuwa na structures/features kama zilizopo kwenye hizi picha zako…

Wadanganye mabwege wa Lumumba kwa Chakubanga.