Tanzania takes delivery of BOEING 787 Dreamliner

IJUE NDEGE AINA YA BOEING 787

Bila shaka umeisikia baada ya Serikali kutangaza kwamba imenunua ndege hiyo lakini hujui muundo wake. Dreamliner ni aina nyingine ya ndege inayotengenezwa na kampuni ya Kimarekani ya Boeing.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 262 na kutembea umbali mrefu bila kusimama.
Tayari Serikali ya Tanzania imelipia malipo ya awali kwa ajili ya uundwaji wa Dreamliner inayotarajiwa kuwasili nchini ifikapo Juni 2018. Ndege hiyo itafanya safari za kimataifa.
Lengo la Serikali kununua ndege hiyo ni kurahisisha usafiri kwa watalii wanaotaka kuja Tanzania kuangalia vivutio vya kitalii. Huenda hiyo ikaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi kikubwa kwa sababu wengi walikuwa wanashindwa kuja kwa kukosa usafiri wa moja kwa moja.
Sifa za Dreamliner
Tofauti na ndege nyingine za ukubwa wa kati, Dreamliner ni ndege inayoweza kwenda umbali wa kilomita 15,200 na kuifanya kuwa ndege yenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi kuliko nyingine.
Ndege hiyo iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza Oktoba 26, 2011 na kusafiri kutoka Tokyo mpaka Hong Kong, inaelezwa kuwa haina kelele kwa asilimia 60 pungufu ya ndege nyingine zenye ukubwa wa aina yake.
Kwa mujibu wa tovuti ya kampuni ya Boeing (www.boeing.com) ndege hiyo ilitengenezwa kwa kumfikiria zaidi abiria. Madirisha ya ndege hiyo ni makubwa kuliko ndege nyingine, ni safi, inaruhusu hewa ya kutosha na ina nafasi ya kutosha mizigo ya kila abiria.
Mtandao huo unaeleza kwamba mpaka sasa zaidi ya watu milioni 125 tayari wamesafiri kwa kutumia Dreamliner kwenda maeneo mbalimbali duniani. Ndege hizo zinasifika kwa kustarehesha abiria kwa sababu zina nafasi kubwa ndani yake na mazingira mazuri.
Ripoti ya shirika la CNN ya mwaka 2011 ilibainisha kwamba ndege ya Dreamliner ni bora kwa biashara ya kusafirisha abiria kwa sababu imezingatia mahitaji muhimu ya kibinadamu ikilinganishwa na ndege nyingine.
Ununuzi wa Dreamliner
Rais John Magufuli alikutana na Mkurugenzi wa Masoko Afrika wa kampuni ya Boeing, Jim Deboo na kufanya mazungumzo kuhusu ununuzi wa ndege hiyo.
Tayari Serikali imenunua ndege sita, mbili aina ya Bombadier Q400 zimewasili nchini wakati ndege nyingine aina hiyo na CS 300 yenye uwezo wa kuchukua abiria 137– 150 zinatarajiwa kuwasili Juni 2017.
Rais alibainisha kwamba ndege ya Boeing 787 Dreamliner itawasili nchini Juni 2018.
“Tayari tumenunua ndege sita, ndege mbili zipo hapa nchini na ndege nyingine zitaanza kuja Juni, mwakani na hiyo Dreamliner itaingia nchini 2018. Ninataka shirika letu la ndege lirudi katika hali yake ya zamani au zaidi,” anasema Rais Magufuli.
http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/ijue-ndege-aina-ya-boeing-787-dreamliner

Sawa mkuu.

ila vipi picha yake umekula?

Fungua link utuwekee. Utamu wa njugu ni kula moja moja.

Naogopa nisije nikaingia TCRA

Jisikie huru kabisa hapa hamna wa kumuogopa.

This is the first generation Boeing 787 aka the troubled 787. Before Tz bought it 3 other customers turned it down. The first generation 787 had problems so most avoided them. That why it cheap at $10 million.

https://www.manufacturing.net/article/2009/09/look-history-troubled-boeing-787

Tanzania

They bought a terrible teen 787 :eek::eek:

This was Boeing first plane that its superstructure was made entirely from carbon fibre and not aluminum. It 30% cheaper and lighter which means less fuel burn. However the first ones developed cracks, forcing airlines to ground most of them. It affected 787 delivery orders for years. KQ was one of them. Boeing compensated all those who had ordered. The first batch made were recalled and fixed however no one took them back. Well Tz has taken up one of them.

Wow @Pascal Mayalla @The Book @Doc Oga na wenzangu wengi hope mumeipata hii. Sitii neno nafikiri mwandishi ameeleza vizuri sana

Ila Juni 2018 ndio hii kwahiyo maatrajio yetu ndege zote zitakua zimefika.

Naona JNIA ikifaidika kwa njia si haba baada ya 787 Kuwasili hivyo basi kuchangia vikubwa katika uchumi wa Tanganyika na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Tatizo mimi sio mbobezi wa haya masaula ya Uchumi, Tusubiri wenyewe waje kutudadavulia ni namna gani tutafaidika kiuchumi. ila kama mleta mada ilivyosema kwamba ndege inaweza kutoka ulaya mpaka Tanzania moja kwa moja bila kuwa na vituo.

Nikusahihishe tu sikuhizi hakuna sehemu inaitwa Tanganyika bali tunayo Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar(Visiwani):cool:

Wa****e nyie. Mzungumze lugha tunaye fahamu sote…@mundu mulosi wapi ile dictionary ya ktalk?

Hivi nyie wenzetu Matusi manaona kawaida sana? au kwavile hamuelewi kiswahili.
Ms***e maana yake ni GAY. hapa kwetu Tanzania hakuna mtu anadharaulika kama mtu mwenye kuingiliwa kinyume na maumbile tena mwanaume

Sasa ni lugha gani hujafahamu humu? kuweni wastaarabu bana

No thus

No this isn’t a terrible teen man

Am starting missing jf already, when you speak like this you have to step proof first forward, eti built entirely from carbon fibers, so where’s the legitimate link to prove your claims.?

So you are trying to say Tanzania bought the neglected aircraft for the cheap price maybe?

Terrible teen? The problem with you is guessing, you are lucky the members of the late JF could not make here all of them but there are some members of the forums who were feeding the forum with all procedures going on inside the Boeing industrial area everything about the aircraft making, behind the scenes (inspectors from the respective ministry)

The great thing about JF was the overcrowded of different experts in every area in every sector, we had the correspondent from Bombardier Canada to Boeing USA

Barafu popote ulipo unahitajika