TBT: Bongo flava

Mjuaji

Village Chief
#3

Amina njoo nikutume kwa kina Aisha
Mwambie Aisha Aje
Kama hataki usimbembeleze
Basi mwambie asije} x 2 (chorus)

Minajua alikuwa ananiambatia
Akaniongopea tunda langu chenza kanihifadhia hui hui hui
Kumbe chungwa kalimenya utadhani chenza
Na lishamegwa na waume wenza ha ha ha ha
Chungwa kalimenya utadhani chenza
Na lishamegwa na waume wenza ha ha ha ha
Bora chenza ngefanisha na limao
Kama si kwa kula ndo ungejua sio
Amina mwambie Aisha aje
Aje na hilo chungwa, aje anipe asiogope, aache mapepe
Basi kama chungwa sitolila kwa nongwa
Basi kama chenza ila nalitunza, lla anipe apunguze mapepe ee ee
Kama hataki usimbembeleze, basi mwambie asije.

(chorus)

Ee najua Hamisa alishamshutukia
Ndio maana akiniona sehemu yoyote nilipo anakimbia ha ha ha ha
Amina mwambie Aisha aje, hata kama ana chungwa, aje hivyo hivyo
Thamani ya mwanamke sio chenza no,
Thamani ya mwanamke ni mwenyewe jinsi alivyo
Wengi wameolewa na machenza, ndoa zao wameshindwa kuzitunza
Na wangapi wameolewa wana chungwa, mpaka sasa ndoa zao wanazichunga
Au basi mwambie asije, huwezi kujua mie ananionaje
Yallah naumia, mi nimeumia, au akinipa mimi nitamkimbia aa
Kwa jinsi mimi ninavyomfagilia aa, Mungu mwenyewe ndio mwenye kujua
Akikubali kwangu msogeze, aje aniliwaze.

(chorus) x 2
 
Last edited:
Top